Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa NEC waombwa kupunguza gharama za fomu za uchaguzi
Habari za Siasa

NEC waombwa kupunguza gharama za fomu za uchaguzi

Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC)
Spread the love

WANANCHI wa kata za tano za wilaya mbalimbali mkoani Morogoro wameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kupunguza gharama za fomu sambamba na kuweka usafiri wa kampeni kwa wagombea walemavu na wanawake ili kuwawezesha kufikia malengo yao ya ushindi kufuatia wengi wao kushindwa mapema. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mafunzo ya kujenga uelewa kwa wadau mbalimbali juu ya uongozi kwa mlengo wa kijinsia yaliyoandaliwa na mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP-Mtandao) kwa kushirikiana na wadau wao wajulikanao kama NORAD washiriki hao akiwemo Abdalia Sultani mkazi wa kata ya Mikese alisema, wagombea wanawake na walemavu katika chaguzi mbalimbali wamekuwa wakikumbwa na changamoto za gharama hizo na kubaki wakitegemea viti maalum kwa wanawake.

Sultani alisema, ifikie mahali sasa Serikali ilione hilo na kupunguza gharama hizo huku wakiondoa nafasi ya viti maalum ambayo imekuwa ikiwalemaza wanawake.

“Gharama za uchaguzi ambazo ni kuchukua fomu huwa ni sh 150,000 kwa Serikali za vijiji, udiwani 50,000 na ubunge 100,000, na gharama za usafiri kwenye kampeni, vimekuwa mwiba kwa wagombea wanawake jambo linalofanya kutokuwa na uwiano au mrengo wa kijinsia katika matokeo ya uchaguzi,” alisema.

Alisema kura za wagombea viti maalum ndizo zinapoteza nafasi za uongoizi kwa kimamama na kwamba kungekuwa mabadiliko ya kutokuwa na viti maalum mapema wanawake wangegombea nafasi kama wanaume.

“Ni lazima wanawake wakubali kushawishiwa kugombea na kuwa na idadi kubwa ya wanawake katika ngazi ya uchaguzi, huku mkiacha dhana ya ‘tukiwezeshwa tunaweza” bali msimame kwa miguu yenu wenyewe,” alisema.

Akizungumzia hilo mshiriki mwingine wa kutoka kata ya kisaki Tatu Mleta aliiomba serikali kutenga bajeti za gharama za usafiri wa kuzunguka kujitangaza kwa wananchi ili kusaidia wanawake ambao wengi wao husindwa kutokana na kukosa kipato.

Naye Afisa Prorgamu wa TGNP-Mtandao, Deoratius Temba aliiomba serikali kuondoa gharama zozote zinazokuwa kikwazo kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu kushiriki kikamilifu kwenye uongozi ikiwemo kuchukua fomu na usafiri kufuatia wengi wao kutokuwa kwenye mfumo wa ajira.

“Kuhusu gharama za kuchukua fomu, tumekuwa tukifuatilia kwa muda mrefu, ili ni suala la kisera, katika nazi ya Taifa na tumekuwa tukizungumza na Serikali juu ya kuangalia namna ya kupunguza,” alisema Temba.

Alisema, marekebisho hayo yatasaidia si kwa uchaguzi wa 2019/20 pekee bali hata kuleta manufaa kwenye chaguzi zijazo.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

error: Content is protected !!