Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Daraja la Salenda kupitia baharini kukamilika 2021
Habari Mchanganyiko

Daraja la Salenda kupitia baharini kukamilika 2021

Daraja la baharini la Salenda
Spread the love

MTENDAJI  Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale amesema, daraja la Salenda linalopitia baharini Coco Beach – Aga Khan, linatarajiwa kukamilika tarehe 14 Oktoba 2021 kama ilivyopangwa. Anaandika Hamis Mguta … (endelea).

Mfugale ametoka kauli hiyo mbele ya Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam aliyefanya ziara ya kutembelea ujenzi huo leo tarehe 19 Juni 2019.

“Mkandarasi amekamilisha asilimia 10 badala ya asilimia 12 ambazo alitakiwa awe amekamilisha kwa awamu ya kwanza katika muda huu, kwasababu alichelewa kidogo kupata vifaa vyake kutoka bandarini.

“Lakini inawezekana akakamilisha daraja hili kabla ya muda kwasababu ya spidi na namna alivyojipanga”, amesema.

Amesema kuwa, mwanzoni mkandarasi anayesimamia ujenzi wa daraja hilo lenye urefu wa Km 1, ambalo kwa sasa lipo katika ukamilishaji wa daraja la muda mfupi, alidhani atafanya kazi kwa saa 12 lakini kwa sasa ameamua kufanya kwa saa 24 ili kazi zifanyike kwa muda wote.

“Amejipanga kwasababu amegawanya kazi ambapo mkandarasi wa awali atakuwa ni kwa ajili ya daraja la pekee na mwengine ni kwa ajili ya barabara,” amesema.

Kwenye ziara hiyo Makonda amesema kuwa, mradi huo unasaidia Watanzania kutokana na ajira za mradi huo na kuwa, hata saruji inayotumika katika ujenzi, inatoka kwenye viwanda vya ndani.

“Leo tunaiona kazi inavyokwenda na kwa hatua na maelezo tuliyopata, tunayo matumaini litakamilika kabla ya muda, nimepata ufahamu wa kutosha juu ya nafasi ya wazawa katika ujenzi wa daraja hili na kunufaika kwao.

“Rais alishaelekeza kuwa, miradi hii iwaache wazawa wakiwa na manufaa na alichokitaka rais hapa ajira kwa wazawa zipo,” amesema.

Amesema kuwa, kwenye mkoa wa Dar es Salaam ndio mkoa pekee ambao haukumpa kura za kutosha Rais John Magufuli mwaka 2015, lakini ndio ambao rais ameupa kipaumbele ili kuufanya unakuwa wa kibiashara.

“Kwenye maandiko matakatifu yanasema, mbaya wako mtendee mema na Rais Magufuli anatenda mema kwa watu ambao hatukumpa kura nyingi, aibu imetukuta wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam,” amesema.

Daraja hilo ambalo linaunganisha Barabara ya Balack Obama na eneo la Coco beach katika makutano ya barabara za Kenyatta na Toure hadi Aga Khan, litagharimu jumla ya Dola za Marekani milioni 112. Pesa hizo zipo tayari kwa ajili ya kukamilisha ujenzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Habari Mchanganyiko

Somo la dini: Waislamu waishukia Serikali, wizara yatoa kauli

Spread the loveJUMUIYA na Taasisi za Kiislamu Tanzania, imetupia lawama Serikali ikidai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!