March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ndugai awashushia vijembe wapinzani bungeni

Spread the love

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo tarehe 15 Novemba 2018 akiwa bungeni jijini Dodoma, amewatania wabunge wa upinzani akiwataka kuvumiliwa kuona wabunge waliohamia CCM wakitokea kwenye vyama vyao, wakisimama bungeni. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo baada ya Mbunge wa Babati mjini aliyetokea Chadema na kuhamia CCM kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli, Pauline Gekul kuuliza swali, ambapo aliwapa pole watani zake na kuwataka wavumilie kitendo hicho alichokiita kuwa ni sindano.

“Watani zangu poleni sana leo mvumilie tu hii sindano,” amesema Spika Ndugai.

Kabla ya kutoa kauli hiyo, Spika Ndugai amesema amemuona Mbunge wa Iringa Mjini kupitia Chadema, Mchungaji Peter Msigwa, ina muuma sana.

Ndugai amesema hayo baada ya Joseph Mkundi, Mbunge wa Ukerewe aliyehamia CCM akitokea Chadema ambacho ni chama cha Msigwa, kwa mara ya kwanza kusimama bungeni kwa ajili ya kuuliza swali.

Vyama vya upinzani hivi karibuni vilikutana na changamoto ya kukimbiwa na baadhi ya wabunge, madiwani na viongozi wake, waliohamia CCM kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kufuatia kuridhishwa na utendaji kazi wa awamu hiyo.

error: Content is protected !!