March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mtolea awahi kabla ya dirisha la usajili CCM kufungwa

Abdallah Mtolea, aliyekuwa Mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CUF

Spread the love

YAMETIMIA. Mbunge wa Temeke, kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Abdallah Mtolea, hatimaye amejiuzulu nafasi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mtolea ametangaza kujiuzulu ubunge na uwanachama wa chama hicho kuanzia leo Alhamisi, tarehe 15 Novemba 2018.

Mbunge huyo amewahi kabla ya muda uliotangazwa na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa leo Novemba 15, 2018 ndiyo mwisho wa kupokea wabunge na madiwani kutoka katika vyama vya Upinzani na baada ya hapo hakuna atakayepewa nafasi ya kugombea tejna nafasi yake.

Mtolea leo ameutangazia umma kutokea bungeni jijini Dodoma kuwa amejiuzulu ubunge na nyadhifa zake zote kwenye chama chake, lakini hakuweka wazi anajiunga na chama gani.Mbunge huyo amesema sababu za kujivua ubunge na nafasi nyingine katika chama chake cha CUF mni kutokana na migogoro inayoendelea katika chama hicho.

error: Content is protected !!