Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kiporo cha Ndugai chapata majibu
Habari za Siasa

Kiporo cha Ndugai chapata majibu

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Marry Mwanjelwa
Spread the love

HATIMAYE swali lililogomewa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu changamoto za baadhi ya watumishi wa umma kutopandishwa madaraja kuanzia mwaka wa fedha wa 2012/13, leo Alhamsi Novemba 15 2018 limepatiwa majibu. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Alhamisi iliyopita Ndugai hakuridhishwa na majibu yaliyotolewa na serikali kuhusu sababu za baadhi ya watumishi kutopandishwa madaraja, na kuelekeza swali hilo lirudiwe tena leo bungeni, ambapo aliiagiza Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kutoa takwimu za watumishi wake waliopandishwa madaraja, ili kubaini ukubwa wa changamoto hiyo na sababu zake.

Baada ya swali hilo kujibiwa, Ndugai amesema takwimu zilizotolewa zinaonyesha kwamba kuna changamoto ya uchelewaji wa watumishi kupandishwa madaraja, ambapo asilimia 50 ya watumishi walioajiriwa Wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI mwaka 2012/13 hawajapandishwa daraja, na kuzitaka mamlaka husika kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo.

“Tulirudisha swali kwa makusudi maalum, zaidi ya watumishi 31,000 walioajiriwa mpaka leo 15,000 wamepandishwa madaraja ina maana 50% wamepanda cheo miaka yote ni mingi sana, eneo hili linahitaji utatuzi na hao ni TAMISEMI na bado hatujapata serikali kuu inabidi hili suala tuliangalie sana,” amesema.

Awali, akijibu swali hilo bungeni jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Marry Mwanjelwa amesema takribani watumishi 31,188 waliajiriwa katika Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI katika mwaka wa fedha wa 2012/13, na 15,320 kati yao walipandishwa madaraja wakati 6,903 wanatarajiwa kupandishwa mwaka huu wa fedha wa 2018/19.

Vile vile, watumishi 1,064 walioajiriwa mwaka 2012/13 hawajapandishwa madaraja kutokana na kuwa na hoja mbalimbali ambazo waajiri wao wanapaswa kukamilisha na kurejesha majina yao wizarani ili wapandishwe vyeo.

Katika hatua nyingine, Mwanjelwa amesema upandishwaji madaraja kwa baadhi ya watumishi hao ulichelewa sababu mwaka ambao walitakiwa kupandishwa 2016/17, serikali ilikuwa na zoezi la uhakiki wa idadi na vyeti vya watumishi wa umma, na kwamba baada ya uhakiki huo serikali ilianza kupandisha madaraja watumishi kwa awamu.

Amesema awamu ya kwanza, watumishi zaidi ya 28,000 walipandishwa madaraja, awamu ya pili watumishi zaidi ya 59,000 walipandishwa na awamu ya tatu watumishi 25,504 walipandishwa, huku wengine wameendelea kukasimiwa kwenye bajeti ya mishahara ili waweze kupandishwa madaraja mwaka huu wa fedha 2018/19.

Katika hatua nyingine, Mwanjelwa aliwaagiza maafisa utumishi kuhakikisha wanawapangia bajeti waajiriwa wao kabla ya kuingia kwenye zoezi la kupandishwa madaraja, sambamba na kuharakisha taariza za watumishi hao wizarani ili zifanyiwe kazi kwa wakati.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!