Wadhamini wakuu wa ligi ya Tanzania bara maarufu kama Ligi ya NBC, Benki ya Taifa ya Biashara(NBC), imewapelekea wakazi wa jiji la Mwanza kombe jipya la ubingwa wa ligi hiyo namba tano kwa ubora barani Afrika. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kwa mujibu wa NBC, lengo la kulipeleka kombe hilo mkoani Mwanza, ni kuwapa fursa wateja wa benki hiyo, wapenzi wa soka na wakazi wa jiji hilo kwa ujumla, fursa ya kulishuhudia na kupiga nalo picha kombe hilo jipya.

Shughuli ya kulishuhudia kombe, imeenda sambamba na fursa ya kupata huduma mbalimbali za kibenki kwa wakazi wa jiji hilo kutoka katika benki hiyo kongwe na yenye mtandao mpana wa matawi hapa nchini.
Leave a comment