Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Nassari ajitetea, aomba huruma ya Spika Ndugai
Habari za SiasaTangulizi

Nassari ajitetea, aomba huruma ya Spika Ndugai

Spread the love

JOSHUA Nassari Mbunge wa Arumeru Mashariki amemtaka Spika Ndugai kupitia upya uamuzi wake ambao haujazingatia ubinadamu na hata kupewa nafasi ya kusililizwa. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa Habari leo kwenye Makao makuu ya Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) leo tarehe 17 Machi mwaka 2019 amesema kuwa bunge wala Spika hawakumpa nafasi ya kumsikiliza kama matakwa ya sheria.

“Hata kama nilifanya makosa yanayostahili adhabu kama hii kwa busara za kawaida nadhani angejiridhisha na kufahamu tatizo langu kwa undani hata kwa nafasi ya kunisikiliza. Hadi sasa sijapokea barua yoyote kutoka ndani ya bunge na nimemjaribu kuwasiliana na Spika  njia ya simu tangu siku ua Alhamisi hado leo hajapokea simu,” amesema Nassari.

Pamoja na Nassari kumuomba huruma ya Spika Ndugai, lakini amekanusha madai ya kuwa yeye hajahudhuria vikao vitatu ambapo amedai kuwa yeye alihudhuria Mkutano wa mwezi Januari.

“Naamini siyo kweli kwa sababu nilikuwa nikihudhuria mikutano ya bunge mfano mzuri nilishiriki shughuli za bunge za Mwezi Septemba. Nikalipwa posho za vikao na stahiki zote kama wabunge wengine,” amesema Nassari na kuongeza:

“Ni kwa muda sasa kwa siku  za usoni hususani Mwezi Novemba na Mwezi Januari ni kweli sikuwepo bungeni lakini kwa sababu ambazo kila binadamu angeweza kuelewa na kuona uzito wake. Ni kwa muda mrefu sasa mke wangu amekuwa na matatizo ya kiafya na sina haja ya kuziongelea kwa undani kwani ni siri kati ya daktari na mgonjwa.”

Amesema kuwa yeye na mke wake tangu walivyooana mwaka 2014 walikuwa wanakiu ya kupata mtoto ambapo walikabiriwa na tatizo la kiafya yaliyowalazimu kwenda nje ya nchi kwa matibabu.

“Kama mume ambaye ninawajibika  nililazimika kusimama na mke wangu na familia yangu na hususani katika siku za mwisho za ujauzito wake mpaka alipofanikiwa kujifungua salama na tukafanikiwa kupata baraka ya mtoto wa kike tarehe 27 mwezi wa kwanza mwaka huu 2019.

“Tarehe 27 ambayo mke wangu amefanikiwa kujifungua mtoto kesho yake tarehe 28 ndio  siku ambayo shughuli za bunge dodoma zilipaswa kuanza,” amesema Nassari.

Amesema kuwa hakuwa na chaguo katika ya kuhudhuria bungeni au kupambania afya ya mke wake.

“Katika hili nilikuwa na machaguo mawili aidha kumuacha mke wangu mahututi ili nihudhurie vikao vya bunge na kamati zake na kusaini posho ama kukisimamia kiapo changu ambacho nilikula kanisani siku ambayo tulioana kwamba nitakuwa na yeye kwenye shida na raha.

“Nilichagua kusimama na familia nikiwa mke wangu ninamshukuru mungu ambaye alikugawia mtoto siku moja kabla ya kikao cha bunge,” amesema Nassari.

Anasema kuwa pamoja na kuwa na hudhuni hii ya kuvuliwa ubunge bila hata kuwepa nafasi ya kujitetea na kuulizwa na spika wabunge kwamba kulikoni bado anamtukuza Mungu na anayoyofuraha ya kupata mtoto kama wanandoa wengine.

“Pamoja na kuwa kwenye changamoto hii ya kuuguza mke kwa miezi hii kadhaa nilifanya juhudi za kuitafuta ofisi ya Spika ili kumjulisha hali halisi nilimjulisha msaidizi wa spika kwa jumbe za maandishi ambazo zipo zilizokuwa nilizungumza naye huyo msaidi wa Spika ambaye anaitwa Saidi Yakubu ambaye ni mtumishi wa bunge,” anasema.

Anasema kuwa baada ya kuzumgumza na mtumishi huyo wa Ofisi ya Bunge  alimpa anuani ya barua pepe ya Ofisi ya Spika na kumhakikishia  kuwa hii ndiyo anauni ambayo Spika atasoma barua yake.

“Barua ambayo nimeituma kwa email haiwezi kufojiwa imeonyesha siku ambayo nimetuma. Kwa hiyo nilimjulisha spika wa bunge kuhusu madhira niliyokuwa nikipitia na nilimjulisha hali ya afya ya mke wangu. Mimi ninamini kuwa Spika anayonafasi ya kupitoa uamuzi wake kma mzazi na mlezi  wa wabunge,” amesema Nassari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!