December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yafanya kweli

Spread the love

Klabu ya Simba imefanikiwa kufuzu katika hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya SC Vital ya Congo katika mchezo ulipigwa kwenye dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea)

Katika mchezo huo AS Vital walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 12 ya mchezo lililofungwa na Kasengu, Simba wakafanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia kwa Mohamed Hussein dakika ya 35na baadae kiungo Clautus Chama aliwapatia Simba bao la ushindi dakika ya 89.

Kwa matokeo hayo Simba atakuwa amefuzu kwenye kundi kama mshindi wa pili baada ya kujikusanyia pointi tisa kwa kushinda michezo yote mitatu ya nyumbani kwenye kundi D, huku kinara wa kundi hilo akiwa ni Al Ahly mwenye pointi 10.

Baada ya bmchezo kumalizika kocha wa klabu ya Simba Patrick Aussems alisema kuwa malengo yao ilikuwa ni kutinga robo fainali ya michuano hiyo na hatimaye wamefanikiwa.

Kabla ya mchezo huo klabu ya SC Vita hawakuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo kwa madai ya kuwa kulipuliziwa dawa ambayo ingeweza kuwamaliza nguvu wakati wa mchezo jambo ambalo walishindwa kuthibitisha.

Tazama video kamili hapo chini

error: Content is protected !!