Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif kuibuka kivingine
Habari za SiasaTangulizi

Maalim Seif kuibuka kivingine

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), yuko mbioni kuondoka chama hicho na kujiunga na moja ya vyama viwili vikubwa vya kisiasa nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Maalim Seif, aweza kuondoka CUF kufuatia serikali ya Chama Cha Mapinduzi, kufanikiwa kumtumia Prof. Ibrahim Lipumba, kumng’oa ndani ya chama hicho.

Taarifa kutoka kwa watu waliokaribu na kiongozi huyo zinasema, hatma ya kisiasa ya Maalim ndani ya CUF, itajulikana mara baada ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam, kutoa uamuzi kwenye shauri lililofunguliwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho wanayemuunga mkono kiongozi huyo.

CUF kimeingia kwenye mgogoro uliokimega chama hicho vipande viwili, kimoja kikiwa kinaongozwa na Prof. Lipumba na kingine kikiongozwa na Maalim.

Chama cha Wananchi (CUF) kimemchagua Khalifa Suleiman Khalifa kuwa katibu mkuu wake mpya kufuatia uchaguzi uliofanywa na baraza kuu la chama hicho.

Jumamosi iliyopita, Prof. Lipumba, mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Francies Mutungi, alimtangaza Khalifa Suleman Khalifa ambaye alipata kuwa mbunge wa Gando, kisiwani Pemba, kuchukua nafasi ya Maalim Seif.

Lipumba alifanya mageuzi hayo ya uongozi, katikati ya zuio la Mahakama Kuu, jambo ambalo linachukuliwa na wachambuzi wa mambo ya kisiasa kuwa lina baraka za serikali.

Aidha, Lipumba ametangaza mabadiliko hayo wakati akiwa ameshafukuzwa uwanachama wa chama hicho na yeye mwenyewe akiwa amewasilisha barua ya kujiuzulu.

Aidha, taarifa zinasema, kinachoitwa “mgogoro” ndani ya CUF ulianza baada ya Prof. Lipumba kuwasilisha barua ya kujiuzulu kama mwenyekiti mwaka 2015 lakini akarejea tena wakati chama kilipokuwa kinajiandaa kumchagua mwenyekiti mpya.

Kuondoka kwa Maalim Seif Sharif Hamad – jabari kuu la kisiasa Visiwani – kunatajwa kuwa kutaongeza nguvu kwa chama chochote cha kisiasa atakachoamua kujiunga nacho.

Mpaka jana Jumapili, tarehe 17 Machi, taarifa zinasema, Maalim anaaweza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) au ACT-Wazalendo.

“Hadi jana Jumapili, kama Maalim Seif ataamua kuondoka, basi anaweza kujiunga ama na Chadema au CUF,” ameeleza mbunge mmoja wa chama hicho na kuongeza, “lakini kwa vyovyote vile, kuna uwezekano mkubwa akajiunga na ACT.”

Maalim Seif amekuwa ndani ya CUF kwa zaidi ya miaka 32 ya uhai wa chama hicho, akianzia kwenye vuguvugu la mabadiliko la KAMAHURU.

Iwapo Maalim Seif atakihama chama hicho, uwezekano wa CUF kuzama kwa kufuata mkumbo wa kilichopo chama kama Tanzania Lebour Party (TLP), ni mkubwa mno.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!