Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Nape: Tumuongezee muda Rais Samia hadi 2030
Habari za SiasaTangulizi

Nape: Tumuongezee muda Rais Samia hadi 2030

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania
Spread the love

 

MBUNGE wa Mtama mkoani Lindi, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amempigia chapuo Rais Samia Suluhu Hassan, akitaka aongezewe muda wa kuiongoza Tanzania hadi 2030. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Nape aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, ametoa kauli hiyo jana tarehe 10 Oktoba 2021, jijini Dar es Salaam, katika kampeni ya ongea na mama, iliyoanzishwa na wasanii nchini Tanzania.

“Kuna wakati tulisema vyuma vimekaza, mama amelegeza sana kama hizi fedha zikienda kule kwenye wakandarasi mzunguko utaongezeka, nawasihi tumuunge mkono mama kwa kazi ambayo ameifanya kwa miezi nane,” alisema Nape.

Nape alisema “tukimpa amalizie hii miaka mitano, tumuongeze na mingine mitano 2025 atupeleke mpaka 2030.

Rais Samia aliingia madarakani tarehe 19 Machi 2021, kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Hayati John Magufuli, kilichotokea tarehe 17 Machi mwaka huu.

Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama

Mwanasiasa huyo amesema, katika kipindi cha miezi nane alichokaa madarakani, amefanya mageuzi mengi yanayogusa maisha ya wananchi wa chini.

“Kimsingi mama anaupiga mwingi sana, kwa kifupi ninachoweza sema mama ameamua kutafsiri ukuaji uchumi kwenye maisha ya watu sababu hizi shughuli nilizotaja zinaenda kugusa shughuli za watu wetu vijijini.”

Nape amesema, awali Jimbo lake la Mtama lilikuwa linapokea Sh. 400 milioni kwa mwaka, kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara, lakini Rais Samia alivyochukua ofisi, jimbo hilo lilipatiwa Sh. 2.3 bilioni.

“Mama katika kipindi cha miezi nane ambayo amekaa madarakani ameshaleta Sh. 2.3 bilioni, maana yake ni mara tano ya fedha iliyokuwa inakuja kwa mwaka mmoja na uongeze milioni tatu. Akitokea mtu ana mashaka ya kumuunga mkono mama, basi huyo ana uwendawazimu wake mwenyewe,” alisema Nape.

Mbunge huyo wa Mtama, alisema tangu Rais Samia ameingia madarakani, malalamiko ya watu kukosa hela mfukoni yamepungua kwa kuwa ameongeza mzunguko wa fedha.

“Kama kwa miezi nane amefanya yote haya, tukimpa miaka 10 itakuwaje. Lakini mama ni msikivu na mwema, baba kidogo alikuwa mkali mkali lakini mama ana ukali kwa wale wanaofanya vibaya lakini ni mpole na ana moyo wa huruma, niwasihi tuendelee kumuunga mkono tumsaidie,” alisema Nape.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Biswalo aendelea kung’ang’aniwa fedha za ‘Plea Bargaining’, CUF wataka ajiuzulu

Spread the love  CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemtaka aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka...

Habari za Siasa

Bunge labaini madudu mfumo ukusanyaji mapato, h’shauri tatu kikaangoni

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

Mkuu wa wilaya ya Rungwe azindua vyumba sita vya madarasa vya thamani ya 64 mil

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amezindua vyumba...

Habari za Siasa

Mbunge afurahia mabilioni ya Samia kutua jimboni

Spread the love  MBUNGE wa Igunga, Nicholas Ngassa ameishukuru Serikali kwa utekelezaji...

error: Content is protected !!