May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mzee Mwinyi atimiza miaka 96, kuzindua kitabu chake leo

Spread the love

 

MZEE Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, leo Jumamosi, tarehe 8 Mei 2021, ametimiza miaka 96. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mwinyi aliyeongoza kwa miaka kumi 1985-1995, alizaliwa tarehe 8 Mei 1925, Kivure, mkoani Pwani.

Anaitumia siku hii ya kuzaliwa kwake, kuzindua kitabu kinachoitwa “Mzee Rukhsa: Safari ya Maisha Yangu” ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.”

Uzinduzi huo, utakaofanyika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, unatarajiwa kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali, akiwemo Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Wengine watakaohudhulia ni; Rais wa Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi, Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete.

Wengine ni marais wastaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume, Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi waandamizi wa sekta mbalimbali ikiwemo wale wa dini, siasa na asaso za kiraia.

Itakuwa ni kitabu cha pili kuzinduliwa, kikitanguliwa na cha Hayati Benjamin Wilium Mkapa, aliyekuwa Rais wa Tanzania kati ya mwaka 1995-2005 , kinachoitwa My Life, My Purpose “Maisha Yangu, Kusudio Langu” kilichozinduliwa tarehe 12 Novemba 2019.

error: Content is protected !!