May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba, Yanga mageti kufungwa Saa 10

Clifford Ndimbo, Msemaji wa TFF

Spread the love

 

IKIWA umebaki muda mchache kabla ya mtanange wa watani wa jadi Simba na Yanga, kupigwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa maelekezo ya kuwa mageti ya Uwanja yatafungwa saa 10:00 ikiwa ni saa moja kabla ya mchezo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo utapigwa leo majira ya saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Simba atakuwa mwenyeji.

Akizungumza suala hilo, Afisa Habri wa TFF, Clifford Ndimbo amesema kwenye mchezo huu wa leo utaratibu utakuwa tofauti kwa kuwa mageti ya Uwanja huo yatafungwa saa moja kabla ya mchezo huo kuanza.

Aidha katika hatua nyingine Ndimbo alisema kwa kuwa mchezo huo umeangukia kipindi cha mwezi wa Ramadhan, wachezaji pamoja na mabenchi ya Ufundi yatapata muda wa kufuturu kwa mchezo kusimamishwa.

Alisema; “Wakati huu tupo kwenye mwezi wa Ramdhan na kuna wachezaji wapo kwenye mfungo kwa hiyo katika mchezo wa kesho kutakuwa na mapumziko mafupi ili kuwapa nafasi wachezaji na benchi la ufundi kupata futari.”

Kabla ya kuingia kwenye mchezo wa leo timu hizo zimekutana mara 107 kwenye mashindano yote, Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi mara 32, huku Yanga ikishinda michezo 37 na wamefanikiwa kwenda sare mara 38.

error: Content is protected !!