May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Guardiolla kutangaza ubingwa mbele ya Chelsea

Pep Guardiolla

Spread the love

 

KLABU ya Manchester City ambayo kikosi chake kipo chini ya Pep Guardiolla huenda leo wakatangazwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu England kama wakifanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya Chelsea. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo utapigwa hii leo kwenye Uwanja wa Etihad jijini Manchester majira ya saa 1:30 usiku.

Endapo Manchester City itaibuka na ushindi kwenye mchezo huo itafikisha jumla ya pointi 83 ambapo hazitaweza kufikiwa na klabu nyingine yoyote kwenye msimamo wa Ligi hiyo.

Wapinzani wa karibu wa Manchester City ni Manchester United ambao wapo kwenye nafasi ya pili ya msimamo wakiwa na pointi 67 na michezo 33.

Kama Manchester United itashinda michezo yake mitano ya itafikisha jumla ya pointi 32.

Endapo Guardiolla atashinda tena taji hili utakuwa ubingwa wake wa tatu toka lipotua kwenye kikosi hiko 2016 akitokea klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani.

Timu hizo mbili mara baada ya mchezo wa leo zitakutana tena kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayochezwa tarehe 28 Mei, 2021, jijini Instabul nchini Uturuki.

error: Content is protected !!