February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mwigulu Nchemba atupwa nje Baraza la Mawaziri

Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani

Spread the love

RAIS John Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri na kumteua Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Lugola kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, nafasi ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na Dk Mwigulu Nchemba. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi amesema mbali na kufanya mabadiliko ya baraza hilo, rais ameteua makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu, mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), makamishna wa tume hiyo na balozi mmoja. 

Balozi Kijazi amesema mbali na uteuzi wa Kangi, Rais Magufuli amemteua mbunge wa Singida Mjini, Mussa Sima kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Pia, amewabadilisha wizara Profesa Makame Mbarawa ambaye alikuwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na sasa amekuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.

Aliyekuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, mhandisi Isaack Kamwelwe ameteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Balozi Kijazi amesema kutokana na umuhimu na uzito wa majukumu katika sekta ya kilimo, Rais Magufuli ameongeza naibu waziri katika Wizara ya Kilimo kwa kumteua mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Omary Mgumba. Kwa uteuzi huo wizara hiyo sasa itakuwa na naibu mawaziri wawili; Mgumba na Dk Mary Mwanjelwa.

error: Content is protected !!