March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Muswada wa Dodoma kuwa Jiji watinga Bungeni

Naibu Spika Job Ndugai

Job Ndugai, Spika wa Bunge

Spread the love

SERIKALI imewasilisha miswada mitano ukiwemo  unaopendekeza kutungwa kwa sheria ya Tamko la Makao Makuu ya mwaka 2018 kwa madhumuni ya kutangaza jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Baadhi ya miswada mingine iliyowasilishwa ni wa marekebisho ya sheria mbalimbali (Na.2) wa mwaka 2018, marekebisho ya sheria mbalimbali (Na.3) ya mwaka 2018, wa sheria ya Bodi ya Kitaalam ya Walimu Tanzania wa mwaka 2018.

Mwingine ni muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya ubia kati ya sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2018.

Akizunguzungumza mara baada ya kusomwa kwa miswada hiyo Spika wa Bunge Job Ndugai alisema itaanza kufanyiwa kazi kwenye bunge lijalo la 11 mkutano wa 12 linalotarajiwa kuanza Septemba 4 mwaka huu.

“Miswada hii mitano imesomwa ukiwemo wa Dodoma kuwa makao makuu ya nchi ambayo tutaifanyia kazi kwenye bunge lijalo, Nawapongeza sana  mawaziri kwa kuuleta maana uliahidiwa miaka mingi sana kulikomingine,” amesema.

Amesema kwa kiasi kikubwa anatumaini kuwa wabunge watautengea haki kwa kuupitisha kwa nguvu ili suala hilo la  Dodoma kuwa makao makuu ya nchi liwe kisheria.

Aliitaka Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa kutambua kuwa wao ndio watashughulikia suala hilo pindi bunge lijalo litakapoanza.

Aidha, amesema muswada miwili  itasimamiwa na Kamati ya Katiba na Sheria, huku mingine miwili inayohusu bodi ya kutathimini ya waalimukisimamiwa na Kamati ya Huduma za Maendeleo ya Jamii.

Pia, Muswada wa ubia kati ya sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2018 ulisimamiwa na Kamati ya Bajeti.

Katika hatua nyingine Spika Ndugai aliwataka wabunge kwenda kuwaeleza wananchi kilichotokea bungeni ukiwemo mjadala wa korosho ambao kwa kiasi kikubwa ulitikisa bunge.

error: Content is protected !!