Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya
Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the love

Mwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela na mahakama ya Marekani kwa kuongoza mtandao wa kimataifa wa ulanguzi wa dawa za kulevya. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Mamlaka za Serikaliya Marekani zimesema Malam Bacai Sanha Jr (52), alipanga kutumia mapato hayo kufadhili azma yake ya kuwa rais wa Guinea-Bissau kupitia mapinduzi.

Sanh Jr ni mtoto wa Malam Bacai Sanha, ambaye aliongoza nchi hiyo ya Afrika Magharibi kutoka 2009 hadi kifo chake mwaka 2012.

Sanha Jr amehusishwa na mapinduzi yaliyofeli mnamo Februari 2022

Alirejeshwa Marekani Agosti 2022, kufuatia kukamatwa kwake nchini Tanzania wiki chache zilizopita.

Kesi yake ilianza kusikilizwa muda mfupi baadaye na Septemba mwaka jana, alikiri kosa la kula njama ya kuingiza dawa za kulevya kinyume cha sheria.

“Malam Bacai Sanha Jr hakuwa mlanguzi wa kimataifa wa dawa za kulevya,” afisa wa FBI Douglas Williams alisema Jumanne.

“Yeye ni mtoto wa rais wa zamani wa Guinea-Bissau na alikuwa akisafirisha dawa za kulevya kwa sababu maalum – kufadhili mapinduzi ambayo hatimaye yangemwezesha kuwa urais wa nchi yake ya asili ambapo alipanga kuanzisha utawala wa madawa ya kulevya.”

Mamlaka ya Marekani inasema Sanha Jr anaweza kufukuzwa nchini humo kufuatia kufungwa kwake kwani yeye si raia wa Marekani.

Sanha Jr anayejulikana kwa jina la “Bacaizinho” nchini Guinea-Bissau, ameshikilia majukumu kadhaa serikalini, ikiwa ni pamoja na kuwa mshauri wa kiuchumi wa babake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!