Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Mwanafunzi kidato cha 3 ajinyonga darasani, akutwa na ujumbe wa kugomea shule
ElimuTangulizi

Mwanafunzi kidato cha 3 ajinyonga darasani, akutwa na ujumbe wa kugomea shule

Spread the love

MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Lumbira kata ya Luanda wilayani Mbozi mkoani Songwe,Japhari Mwashitete  (16) amekutwa amefariki dunia kwa kujinyonga darasani.

Mwili wa mwanafunzi huyo umekutwa ukiwa na ujumbe wa  kuikataa shule hiyo. Anaripoti Ibrahim Yassin…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jana tarehe 4  Julai 2023, Kamanda wa polisi mkoani Songwe, Theopista Mallya amesema wamepokea taatifa za kuiinyonga mwanatunzi huyo juzi tarehe 3 Julai 2023 muda wa saa 10 jioni.

RPC Mallya

Amefafanua kuwa polisi walifanya taratibu za vipimo vya daktari na kubaini amekufa kwa kujinyonga hivyo polisi wakaamua kuruhusu familia kuendelea na taratibu za mazishi. 

Kamanda Malya amesema baada ya kifo hicho waliangalia kwenye mfuko wa suruali ya mwanafunzi huyo na kukuta karatasi yenye maandishi yenye ujumbe wa kukataa kusoma shule ya Lumbira na badala yake anataka kusoma shule ya Myovizi iliyopo kilometa chache kutoka shule hiyo

Amesema kufuatia tukio hilo hakuna mtu ama watu waliokamatwa wakihusishwa na tukio hilo huku jeshi lake likiendelea na uchunguzi wa kina kuona kama kuna mtu ama watu wamehusika na tukio hilo. 

Kufuatia tukio hilo wananchi wanaozunguka eneo hilo wamesikitishwa na kitendo cha mwanafunzi huyo kuchukua maamuzi hayo magumu huku wakitaka uchunguzi zaidi ufanyike kuona kama kuna mtu kahusika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Viwanda zaidi ya 200 kuonyesha bidhaa maonyesho ya TIMEXPO Dar

Spread the loveSHIRIKISHO la Wenye Viwanda Nchini (CTI) kwa kushirikiana na Mamlaka...

Elimu

Wazazi wa wanafunzi waliokosa nafasi vyuo vikuu waonyeshwa njia na GEL

Spread the loveWAKALA wa Elimu ya Vyuo Vikuu Nje ya Nchi, Global Education...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

error: Content is protected !!