May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwalimu wa madrasa ahukumiwa miaka 80 jela kwa ubakaji

Spread the love

 

MUSSA Nassibu Ismail (21), mwalimu wa madrasa iliyopo maeneo ya Kiboje wilayani Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, amehukumiwa kifungo cha miaka 80 gerezani au faini ya Sh. 3,000,000, baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa kike wa miaka 15. Anaripoti Noela Shila, TUDARCO … (endelea).

Hukumu hiyo imetolewa jana tarehe 17 Agosti 2021 na Mahakama ya Mkoa wa Mwera visiwani Zanzibar, mbele ya Hakimu Said Hemed Khalfan.

Akitoa hukumu ya kesi hiyo iliyokuwa na mashtaka manne, Hakimu Khalfan amesema mshtakiwa huyo amehukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa kila kosa, katika mashtaka mawili ya ubakaji yanayomkabili.

Huku, akihukumiwa kifungo cha miaka 10 kwa kila kosa, katika mashtaka mawili yanayomkabili ya kumtorosha mtoto huyo.

Hivyo, jumla ya muda wa kifungo ni miaka 80, lakini mshtakiwa huyo atatumikia kifungo cha miaka 30 pekee, kwa kuwa adhabu hiyo inakwenda kwa pamoja.

Hakimu Halfani alisema, mshtakiwa huyo alifanya makosa hayo kati ya Oktoba 18 na Novemba 2, 2019, katika madrasa iliyoko maeneo ya Kiboje visiwani humo.

error: Content is protected !!