Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Simbachawene: Hatutahuisha usajili taasisi za dini
Habari Mchanganyiko

Waziri Simbachawene: Hatutahuisha usajili taasisi za dini

Spread the love

 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, George Simbachawene amesema shughuli ya mabadiliko ya hadhi ya vyeti vya usajili wa jumuiya utahusisha vyama vya kijamii pekee badala ya taasisi za kidini. Anaripoti Mwanaharusi Abdallah, TUDARCo … (endelea).

Uamuzi huo umetolewa jana Jumanne tarehe 17 Agosti 2021 jijini Dodoma wakati wa kikao cha Waziri Simbachawene na viongozi wa mabaraza ya kidini na mashirikisho ya dini mbalimbali nchini humo.

Tarehe 10 Agosti 2021, wizara hiyo ilitoa taarifa ya mabadiliko ya hadhi ya vyeti vya usajili wa taaisi za kidini na jumuiya mbalimbali za kijamii.
Mabadiliko hayo yalitoka kuwa vya kudumu na kuwa vya kuhuisha kila baada ya miaka mitano.

Lengo ni kufanya tathimini ya jumuiya zote zilizo hai nchini na kuhakiki utii wa masharti ya usajili pamoja na matakwa ya sheria ya jumuiya zote zilizo nchini.

Taarifa hiyo ya Msajili wa Jumuiya, Emmanuel Kihampa alizitaka taasisi zote ofisini kwake jijini Dodoma kwa lengo la kuhuisha.

Hata hivyo, jana Jumanne, Waziri Simbachawene alibadilisha uamuzi huo baada ya majadiliano kati yake na viongozi wa taasisi za kidini.

“Tumeona kuwa ni vyema kwa sasa zoezi hili likahusisha Jumuiya za Kijamii 8,851 tu na halitahusisha taasisi za kidini, hadi pale Serikali itakapoamua vinginevyo,” alisema Simbachawene.

Waziri Simbachawene alisema jumla ya vyama vya kijamii 8,851 ndizo zitakazohusishwa katika shughuli inayoendelea hivi sasa, kupitia Ofisi ya Msajili wa Jumuiya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kwa upande wake, Msajili wa Jumuiya, Emmanuel Kihampa alisema kufuatia mabadiliko hayo, vyama vyote vya Kijamii nchini vinaagizwa kufika katika Ofisi ya Msajili wa Jumuiya iliyopo Ghorofa ya 11 katika Jengo la Kambarage Jijini Dodoma, kwa lengo la kuhuisha usajili wake na kupatiwa vyeti vipya vya usajili.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Wailsamu Tanzania (Bakwata), Shekhe Hamis Mataka alimshukuru Waziri Simbachawene pamoja na uongozi wa wizara kwa kukutana na viongozi wa dini katika mkutano huo.

“Leo tunafuraha, Waziri upo, Naibu Waziri, Katibu Mkuu pamoja na Msajili wetu, hii inatusaidia hata migogoro mbalimbali yakidini inayokusumbua mheshimiwa Waziri kwa kukutana huku kunakusaidia endapo itatengenezewa njia kupitia kukutana katika umoja huu,” alisema Shekhe Mtaka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa

Spread the loveKiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza...

Habari Mchanganyiko

NMB yafuturisha Dar, Majaliwa azitaka Serikali za Mitaa, Taasisi zijifunze kwao

Spread the loveBENKI ya NMB imewafuturisha wateja wake walio kwenye Mfungo wa...

error: Content is protected !!