March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mwakyembe atoa sababu 10 za kuhamia CCM

Spread the love

ALIYEKUWA Diwani wa Mtoni kwa tiketi ya CHADEMA, Bernard Mwakyembe, ametoa sababu 10 zilizomfanya aondoke Chadema na kuhamia CCM. Anaripoti Gerva Lyenda … (endelea).

Mwakyembe alizitaja sababu hizo mbele ya Waandishi wa habari leo Jumamosi tarehe 29 Septemba kwenye mkutano na vyombo vya habari alioufanya jijini Dar es Salaam.

Mwakyembe alizitaja sababu hizo kuwa ni kasi ya kufanya maendeleo inayofanywa na Serikali, agenda za Chadema kutekelezwa na Serikali, kujengwa miundombinu, ujenzi wa mradi wa Stigler’s Gorge, reli ya standard gauge na kushughulika na mafisadi kunakofanywa na Serikali.

Alizitaja sababu nyingine kuwa ni kuondolewa watumishi hewa makazini, ununuzi wa ndege, kupunguza matumizi ya Serikali na kuboresha huduma za hospitali ya Muhimbili ambapo sasa watu hawaendi nje ya nchi kutafuta matibabu bora.

Mwanasiasa huyo anayedai kuwa alikuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alijiunga na CCM Septemba 15 mwaka huu.

error: Content is protected !!