Sunday , 2 April 2023
Home Kitengo Michezo Cristiano Ronaldo atuhumiwa kwa ukatili wa ngono
Michezo

Cristiano Ronaldo atuhumiwa kwa ukatili wa ngono

Spread the love

MWANAMKE mmoja kutoka jimbo la Las Vegas nchini Marekani, Kathryn Mayorga ameibuka hadharani na kumtuhumu nyota wa mpira wa miguu duniani, Cristiano Ronaldo kwamba alimfanyia ukatili wa kingono kwa kumbaka mwaka 2009. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Katika mashtaka yake aliyofungua Ijumaa ya tarehe 28 Septemba 2018, Mwanadada huyo alidai kuwa, Ronaldo alimfanyia ukatili huo alipokutana naye katika hoteli ya ‘The Palms and Casino’ iliyoko Las Vegas mnamo Juni 13 2009. Na kwamba baada ya kufanya kosa hilo, Ronaldo alimtaka radhi.

Mayorga alidai kuwa, Ronaldo pamoja na timu yake walimshinikiza kupokea kiasi cha dola za kimarekani 375,000 ili anyamaze kimya.

Hata hivyo, Ronaldo kupitia ukurasa wake wa Instargram mwishoni mwa wiki alikana madai hayo akisema kuwa ni taarifa za uongo na kwamba walengwa wanataka kupata umaarufu kupitia jina lake.

Naye Wakili wa Ronaldo, Chriastian Schert alikana mashtaka hayo akidai kuwa madai hayo yanakiuka haki za mteja wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

TANROADS wawataka watumishi wazingatie michezo kazini

Spread the love  WAKALA wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema michezo inapaswa kuzingatiwa...

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

error: Content is protected !!