Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya
Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Freeman Mbowe
Spread the love

MKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), uliokuwa unafanyika kwenye Viwanja vya Ruanda Nzovwe, umeahirishwa baada ya mvua kubwa kunyesha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya…(endelea).

Tukio hilo limetokea leo Jumanne, tarehe 20 Februari 2024, jijini Mbeya, baada ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, kuuahirisha muda mfupi baada ya mkutano huo kuanza ambapo viongozi wakuu wa chama hicho walikuwa hawajaanza kuzungumza.

Mkutano huo ulifanyika baada ya Chadema kufanya maandamano kuanzia asubuhi ya leo, ambapo ilipanga kuyahitimisha kwa kufanya mkutano huo wa hadhara.

Maandamano Chadema

“Kazi kubwa iliyotuleta Mbeya leo ilikuwa ni maandamano, kazi ambayo tumeimaliza ahsanteni sana, kwa hali ya hewa ilivyo na kwa namna ambavyo wanaharibiwa kamera zao wanahabari wetu ni naomba kwa leo tumshukuru Mungu angalau yameweza kutoka Mbalizi na Uyole mpaka hapa, hiyo ni Baraka kubwa sana kwa Mungu,” amesema Mbowe na kuongeza

“Kwa maana hiyo mkutano wetu wa hadhara kwa siku ya leo hautaendelea, tutatangaza tarehe mpya ya siku nyingine tutazungumza kwa muda mrefu.”

Awali, watu kadhaa walipata nafasi ya kuzumza akiwemo  aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa, aliyesema ameunga mkono maandamano hayo ili kudai katiba mpya na kuishinikiza serikali itatue changamoto ya ugumu wa maisha.

“Katiba ya leo tuliyo nayo tunaita katiba ya 1977 ilitengenezw a na watuw asiozidi 20 kwa siku chache, hakuna sababu leo Samia na Serikali yake kutuambia muda hautoshi tunataka kumwambia Samia, katiba ni mali ya watanzania kama alichaguliwa kwa mujibu wa katiba lazima aiheshimu na kuitii katiba. Tunaungana na Chadema na tutaungana na asasi na wale wanaopigania kupunguza gharama za maisha na wanaopambana tupate katiba mpya,” amesema Slaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

error: Content is protected !!