February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Muswada wa kutambua madaktari wapitishwa

Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Spread the love

BUNGE limeridhia na kupitisha  muswada wa sheria ya madaktari, madaktari wa meno na wataalam wa afya shirikishi wa mwaka 2016, ambao utasimamia taaluma na maadili ya wanataaluma wa sekta ya afya ili kulinda usalama wa afya kwa Watanzania, anaandika Dany Tibason.

Pia serikali inatarajiwa kupeleka bungeni muswada  ambao utamlazimisha kila Mtanzania kuwa na bima ya afya kutokana na umuhimu wake katika suala la afya.

Akijibu hoja za wabunge waliochangia muswada huo, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema sababu ya kupelekwa kwa muswada huo ni  kutokana na kuwa na ongezeko la wataalam, ambapo hivi sasa Tanzania wanazalisha zaidi ya madaktari 1000 kwa mwaka na kuwa moja ya nchi zinazoongoza kwa  idadi kubwa ya watalaam hao.

error: Content is protected !!