Monday , 4 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Msomi asema Tanzania haina dira
Habari Mchanganyiko

Msomi asema Tanzania haina dira

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ruaha Prof. Gaudens  Mpangala
Spread the love

WADAU wa Jukwaa la Katiba Tanzania wamesema kuwa taifa haliwezi kuwa na maendeleo kama halitakiwa na dira ya maendeleo inayoeleweka,” anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ruaha Prof. Gaudens  Mpangala wakati wa mafunzo ya wanachama wa Jukwaa hilo kuhusu hatma ya mchakato wa Katiba Mpya Tanzania.

Licha ya kuwa Tanzania  haina dira kwa sasa pia Mhadhiri huyo amesema bila kurudisha mchakato wa Katiba Mpya ya Tanzania, yenye maoni ya  wananchi hakuna maendeleo ambayo yanaweza kupatikana.

Prof.  Mpangala amesema kuwa kwa sasa hali ya demokrasia imeminywa na kwamba  wananchi hawana maamuzi yoyote.

Amesema demokrasia iliyopo kwa sasa ni kupiga kura, lakini baada ya kumalizika kwa uchaguzi Watanzania wengi wamekuwa hawana demokrasia hatua inayosababisha washindwe  kujieleza au kukosoa mambo mbalimbali ambayo yanatakiwa kuhojiwa.

“Lazima kujua kuwa kuna nguzo tatu za demokrasia ambazo ni Mamlaka ya wananchi, Ushiriki wa wananchi pamoja na Ukombozi kwa wananchi”amesema

Prof  .Mpangala amesema kwa sasa haki za binadamu hazifuatwi kwa kuwa yapo mambo ambayo yanaendelea kujitokeza ikiwa ni pamoja na Mahakama na Bunge kuingiliwa badala ya vyombo hivyo kusimamia haki ambazo zinatakiwa.

Amesema inafahamika wazi kuwa Bunge linatakiwa kuisimamia serikali lakini kwa bahati mbaya kwa sasa serikali imekuwa ikilisimamia jambo ambalo si la Kidemokrasia.

“Tunajua wazi kuwa kwa sasa serikali ya awamu ya tano inaonesha wazi kuwa inataka maendeleo ya haraka, lakini kuwa na maendeleo bila kuwa na dira na demokrasia ya kweli haiwezekani.

“Huwezi kusema uchumi umekuwa wakati wananchi ni maskini, ili uweze kusema kwamba uchumi umekuwa ni lazima uwe na watu ambao si maskini na wana uwezo wa kupata mahitaji yao ya lazima,” amesema.

“Tanzania hakuna dira tunaenda wapi? kumbuka mwanzoni kulikuwa na Azimio la Arusha hiyo ilikuwa ni dira ya kulifanya taifa kujua wapi linakwenda lakini kwa sasa tunayumba daraja kati ya maskini na matajiri ni kubwa mbaya zaidi wapo vijana wengi wenye elimu lakini hawana ajira.

“Juhudi zote nzuri za  awamu ya tano bila kuwa na dira ni bure hata hivyo dira ya nchi inatokana na Katiba mpya ambayo  inatokana na rasmu ya maoni ya wananchi ya Jaji Mstaafu  Joseph  Warioba na si vinginevyo,” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Hebron Mwakagenda, amesema kuwa haiwezekani serikali ikatumia fedha za walipa kodi zaidi ya bilioni 100 kwa ajili ya mchakato wa katiba halafu isipatikane.

Amesema Jukwaa la Katiba ya Tanzania ,ni kuhakikisha inawaamsha Watanzania pamoja na Asasi mbalimbali ili kudai katiba ya wananchi ambayo inatokana na maoni yao.

Katika hatua nyingine Mwakagenda amesema jukwaa hilo limemwandikia barua nne rais John Magufuli, lakini hajajibu hata moja hadi leo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

TEF yaomboleza kifo cha Mzee Mwinyi

Spread the loveJukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeeleza kupokea kwa masikitiko taarifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

Maambukizi ya UKIMWI Lindi yapungua

Spread the loveMaambukizi ya Virusi vya UKIMWI yamepungua katika Manispaa ya Mkoa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mgomo kitita kipya cha NHIF: Serikali yaita hopsitali binafsi mezani

Spread the loveSERIKALI imekiita mezani Chama cha Wenye Hospitali Binafsi (APHFTA), ili...

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

error: Content is protected !!