Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Msajili aionya Chadema, Prof. Safari aduwaa
Habari za SiasaTangulizi

Msajili aionya Chadema, Prof. Safari aduwaa

Profesa Abdallah Safari,makamu mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

HATUA ya Frederick Sumaye, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (Chadema), Kanda ya Pwani kuangushwa kwenye uchaguzi wa kanda hiyo, imemshtua Prof. Abdallah Safari, makamu mwenyekiti wa chama hicho. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Wakati mvumo wa mizengwe kutumika kumwangusha Sumaye ukishika kasi, Ofisi ya Msaji wa Vyama vya Siasa imeonya, kwamba kuna hatari ya viongozi wa juu kutotambuliwa na ofisi hiyo, iwapo itajiridhisha kanuni za uchaguzi huo zimebakwa.

Uchaguzi wa ndani wa chama hicho katika ngazi mbalimbali unaendelea nchini, ambapo tamati ya uchaguzi huo inatarajiwa kuwa tarehe 18 Desemba 2019, pale viongozi wakuu wa chama hicho watakapopatikana.

Prof. Safari akizungumza na mtandao huu, ameonesha kushangazwa baada ya Sumaye kuangushwa kwenye uchaguzi huo uliofanyika tarehe 28 Novemba 2019.

“Ninavyomjua Sumaye na jinsi alivyo lulu kwenye chama hiki, Chadema kimepoteza lulu kwenye kanda hiyo. Sumaye ni muungwana, mwadilifu na mwenye uwezo mkubwa kwenye uongozi.

“Nawatahadharisha Chadema pia nawaonya kwamba wanacheza na lulu. Naona wanazungumzia demokrasia lakini nashangaa kwanini hawawajui watu wenye weledi, uwezo mkubwa na mawazo chanya katika kuongoza. Sielewi kwanini hili halionekani ndani ya chama,” amesema Prof. Safari.

Prof. Safari ambaye ni mwanasheria mkongwe amesema, anatarajia kuendelea na maisha yake baada ya kukabidhi nafasi yake ya umakamu mwenyekiti kwa viongozi wajao.

Sisty Nyahoza, Naibu Msajili katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, ametahadharisha Chadema kuzingatia kanuni za uchaguzi.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari nchini, Nyahoza kwa niaba ya msajili wa vyama amesema, ofisi yake haitaona tabu kutotambua viongozi watakaochaguliwa pale itapojiridhisha kama mbinu hasi zilitumika.

Tarehe 18 Novemba 2019, chama hicho pamoja na mambo mengine, kinatarajiwa kupata viongozi wake wakuu akiwemo mwenyekiti Taifa.

Hata hivyo, unapofika katika kuwania uenyekiti wa chama hicho mwaka 2004, demokrasia huyumba na kumfanya Mbowe aendelee kuwa mwenyekiti.

Waliowahi kujitokeza kuchuana na Mbowe akiwemo Chacha Wange na Zitto Kabwe, waliishia njiani. Kwenye kinyang’anyiro cha sasa, Mbowe atavaana na Sumaye pia Cecil Mwambe (Mbunge wa Ndanda).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!