September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mrithi wa Nassar akabidhiwa jimbo

Dk. John Pallangyo, Mbunge wa Arumeru Mashariki

Spread the love

MRITHI wa Joshua Nassari katika Jimbo la Arumeru Mashariki, Dk. John Pallangyo, ameapishwa leo tarehe 22 Mei 2019 kuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Job Ndugai, Spika wa Bunge amemwapisha Dk. Pallangyo, kabla ya kuapishwa kwake, alisindikizwa kwa mbwembwe na wabunge wa CCM huku wakiimba nyimbo za chama hicho.

Baada ya kula kiapo, mbunge huyo alianza kusalimia baadhi ya wabunge ambapo alianza na Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu na wabunge wengine wa CCM,

Baada ya hapo, alikwenda upande wa upinzani na kumsalimia na kuteta kidogo na John Mnyika, Mbunge wa Kibamba na Joseph Selasin, Mbunge wa Rombo.

Dk. Pallangyo amekuwa mbunge bila kupigiwa kura. Ni baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwaengua wagombea wa vyama vingine kwa madai ya kutokuwa na sifa.

Nassari alig’olewa kwenye nafasi hiyo baada ya Spika Ndugai, kumsimamisha kutokana na kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge mfululizo bila kutoa taarifa.

error: Content is protected !!