Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mpina anyukana bungeni na Mwigulu, ataka ashtakiwe kwa uhujumu uchumi
Habari za SiasaTangulizi

Mpina anyukana bungeni na Mwigulu, ataka ashtakiwe kwa uhujumu uchumi

Luhaga Mpina
Spread the love

MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, ametaka Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa na Mkurugenzi Mtendaji wa TRC, Masanja Kadogosa, wafunguliwe mashataka ya uhujumu uchumi akidai wamefanya ubadhirifu katika mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa  (SGR), roti ya tatu na nne. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Akizungumza bungeni jijini Dodoma, leo tarehe 3 Novemba 2023, Luhaga amedai kuwa ufisadi huo umetokana na uamuzi wa viongozi hao kutoa zabuni ya mradi huo kwa Kampuni ya Yerp Merkez, bila kuishindanisha na kampuni nyingine, kinyume na sheria inayotaka tenda zigawanywe kwa ushindani.

Mpina amedai kuwa, Dk. Mwigulu kupitia katibu mkuu wake, aliandika barua kutaka mkataba kati ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Kampuni ya Yapi Merkezi, usainiwe licha kukiuka sheria kwa madai kwamba uamuzi huo ulilenga kuisaidia Serikali kupata mkopo kutoka Benki ya Standard Chatered.

Katika hatua nyingine, Mpina amedai kuna ongezeko la gharama za mradi huo katika roti ya tatu na nne, akidai kuwa linatokana na upigaji uliofanywa na baadhi ya viongozi.

“Kamati ya Bunge inakiri kwamba, Serikali ilipoacha utaratibu wa njia ya ushindani katika kutafuta mzauni, ilipata ongezeko la Dola za Marekani 5 milioni sawa na Sh. 3 bilioni kwa kila mita moja ya SGR. Wakati inatumia njia ya ushindani gharama ya kilomita moja ya SGR iliongezeka kwa Sh. 0.45 bilioni,” amesema Mpinga.

Katika hatua nyingine, Mpina alidai usalama wa fedha za umma haupo, kutokana na uwepo wa taarifa shuku za fedha kiasi cha Sh. 280 trilioni, zinazodaiwa kuhamishwa ndani na nje ya nchi.

Baada ya Mpina kutoa madai hayo, Dk. Mwigulu alisimama kwa ajili ya kutoa ufafanuzi, ambapo alianza na tuhuma za fedha zinazodaiwa kuwa zimepotea, akisema taarifa hizo ni za miamala shuku iliyofanywa na sketa binafsi na sio uhamisho.

“Huo sio uhamisho ni shughuli za kila siku zinaenbdelea na hatuwezi zuia shughuli katika nchi, kwa ahiyo sio wizi wala sio uhamisho wa fedha ambazo zinatoka hazina ama idara ya serikali kwenda mahali fulani, ni shughuli za kiuchumi. Ukisema umepigwa trilioni 30 sio sahihi wakati bajeti ya nchi hatujafika hata trilioni 50,” amesema Dk. Mwigulu.

Kuhusu mradi wa SGRA, Dk. Mwigulu alitoa ufafanuzi akisema “hakuna mkopo wowote hapa nchini umewahi kuchukuliwa kwa kuvunjwa sheria, mikopo yote inayochukuliwa imepitishwa kwenye bajeti na bunge hili na inafuata taratibu zote za ukopaji.”

Naye Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, alisimama kumjibu Mpina kuhusu madai ya ongezeko la fedha za mradi akisema “nilitaka nitoe ufafanuzi kipi kinapelekea ongezeko hili. Nimezungumza hapa kwa muda mrefu sababu iliyopelekea kutofautiana kwa fedha kati ya roti 1,2,3 na 4.”

“Ziko sababu nyingi na moja ukiangalia kwenye roti 3 na 4 ilikuwa na lift Valey kilomita 50. Ilikuwa na muunganiko, pale kuna karakana, chuo cha reli wakati haya yote kule roti 1 na 2 hayakuwepo. Pia, kuna ujenzi wa kituo kikubwa kinachoenda Kigoma mpaka Tanganyika,” amesema Kihenzile.

Licha ya ufafanuzi huo, Mpina alikataa kupokea taarifa akidai waliosimama kumjibu walilenga kupoteza muda wake bure.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!