Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Msukuma aibua sakata la IPTL bungeni
Habari za SiasaTangulizi

Msukuma aibua sakata la IPTL bungeni

Joseph Kasheku 'Msukuma,' Mbunge wa Geita Vijijini
Spread the love

MBUNGE wa Geita Vijiji, Joseph Kasheku maarufu kama Msukuma, amehoji kwa ajili sakata la Tegeta Escrow haliishi baada ya Kampuni ya IPTL inayohusishwa na suala hilo, kuibukia mahakamani kutaka Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), iliipe fedha zilizotokana na utekelezaji mkataba wa kuzalisha umeme. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Msukuma amehoji hayo bungeni jijini Dodoma, leo tarehe 3 Novemba 2023, akizungumzia ubadhirifu wa fedha za umma unaoripotiwa na ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), bila wahusika kuchukuliwa hatua.

Mwanasiasa huyo amedai, ameanza kusikia sakata hilo kabla hajawa mbunge, lakini anashangaa hadi leo IPTL inataka ilipwe fedha.Msukuma alianza kuwa mbunge 2015 ambao anahudumu kwenye nafasi hiyo hadi sasa.

“Nataka kuzungumza kuhusu IPTL, hii IPTL toka Christopher Olesendeka alikuwa kioo change anahangaika mpaka lep. Watu wakasema hela ya mboga zikalipwa. Leo tena kizazi chetu ameibuka anataka kulipwa, ni dalili gani hizi jamani? Hizi hela zinapelekwa wapi? Kwa sababu hela ni nyingi mno zinatajwa kuibiwa mbona kwenye mabenki mzungukoni hazimo?” amehoji Msukuma.

Katika hatua nyingine, Msukuma ameitaka Serikali kuwachukulia hatua watu watakaobainika kuhusika kwenye ufisadi uliotajwa katika ripoti za CAG.

Sakata la Escrow lilishika kasi 2013, ambalo liliibua mvutano bungeni juu ya uhalali wa kuchotwa fedha kiasi cha Sh. 320 bilioni, kwenye akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwa ajili ya kumaliza mgogoro kati ya TANESCO na IPTL.

Mnamo 2021, IPTL kupitia mwanasheria wake, Joseph Makandege, ilipinga sakata hilo kujadiliwa bungeni jijini Dodoma, kwa madai kuwa wanaolijadili vibaya wana mgongano wa kimaslahi.

IPTL inayomilikiwa na Harbinder Singh Sethi, inadaiwa kufungua kesi mwaka huu, ikiitaka TANESCO iilipe mabilioni ya fedha, ikidai ilikiuka makubaliano waliyoingia ya uzalishaji na ununuzi wa umeme.

Hata hivyo, kesi hiyo inadaiwa kuendeshwa katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu, jijini Dar es Salaam, kimya kimya baada ya IPTL kuomba iendeshwe kwa siri ikidai taarifa zake zimekuwa zikipotoshwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

error: Content is protected !!