Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mpango wa kuajiri mwanamke kushika mimba wafufuliwa
Habari MchanganyikoKimataifa

Mpango wa kuajiri mwanamke kushika mimba wafufuliwa

Spread the love

SERIKALI ya Thailand imepanga kufufua mpango wa wa biashara ya mwanamke kukubali kushika mimba na kujifungua mtoto kwa niaba ya familia fulani maarufu kama ‘Surrogacy’. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Mpango huo umerejea tena baada ya zoezi hilo kupigwa marufuku karibu muongo mmoja uliopita kutokana na mfululizo wa kashfa za usafirishaji haramu wa watoto na wanawake walioajiriwa kushika mimba hizo.

Mkuu wa idara inayotoa msaada wa huduma za afya katika Wizara ya Afya ya Umma nchini humo, Sura Visetsak ametangaza mpango huo mapema mwezi huu kwamba rasimu ya sheria ya kuhalalisha biashara hiyo imeshakamilika.

Amesema biashara hiyo “Surrogacy” itawahusu wanandoa wa ndani na wa nje ya Thailand kwa lengo la kuleta mageuzi yatakayobadili kiwango cha uzazi kinachopungua nchini humo. Hadi sasa nchi hiyo ina idadi ya watu milioni 71.

Hata hivyo, Sunwanee Dolah ambaye anatoa ushauri kwa makundi ya ndani kuhusu biashara ya binadamu na masuala ya haki za wanawake amesema bado kuna wasiwasi mkubwa kuhusu biashara hiyo.

“Huenda watu wengi watakuwa waathirika wa biashara ya usafirishaji binadamu, au watalazimika kutoa huduma hiyo kama biashara ya Surrogacy, itahalalishwa,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!