Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Cheyo: Mkitaka kufilisika ingieni kwenye siasa, wenye pesa wezi
Habari za Siasa

Cheyo: Mkitaka kufilisika ingieni kwenye siasa, wenye pesa wezi

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha UDP, Mzee John Cheyo, amewaasa vijana wenye nia ya kuingia katika siasa kwa ajili ya kutafuta pesa, wasifanye hivyo kwani watafilisika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza katika kongamano la majadiliano ya viongozi wa vyama vya siasa, lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), leo Jumatatu, jijini Dar es Salaam, Mzee Cheyo amedai katika siasa hakuna pesa na kwamba baadhi ya wenye pesa ni wezi.

Mwenyekiti wa Chama cha UDP, Mzee John Cheyo

“Nataka kuwaasa vijana, tumepewa tafsiri mbovu ya uongozi pesa ndugu yangu kama unataka kufilisika katika maisha yako nenda kwenye siasa. Mawazo kwamba utapata pesa kwenye siasa, hakuna pesa na wale mnaowaona wana pesa ni wezi tu. Nikiangalia hapa sioni kijana anayetaka kuwa mwizi naona mnataka kusaidia watu endeleeni na fikra hizi,” amesema Mzee Cheyo.

Mzee Cheyo amesema uongozi mtu anazaliwa nao na kwamba wale wanaojiona wana wito wa uongozi wakipata nafasi waitumie kubadilisha maisha ya watu wanaowaongoza yawe mazuri.

“Kama unataka kuwa mwanasiasa lazima uwe na ule moyo wa kusaidia watu, uwe na ule moyo wa kujaribu kubadilisha mambo ya watu,” amesema Mzee Cheyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!