Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kiongozi mkuu upinzani Burundi ang’olewa kwenye chama
Habari za SiasaKimataifa

Kiongozi mkuu upinzani Burundi ang’olewa kwenye chama

Agathon Rwasa
Spread the love

Chama kikuu cha upinzani nchini Burundi kimekumbwa na mgawanyiko baada ya jana Jumapili kusema kuwa limemuondoa madarakani kiongozi wa chama hicho Agathon Rwasa kwa kushindwa kuunganisha pande mbili zinazolumbana. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea)

Rwasa aliondolewa kwenye uongozi na tawi la chama cha National Freedom Council (CNL) katika kongamano la chama kaskazini mwa nchi.

Taarifa kutoka nchini humo zinasema nafasi ya kiongozi huyo wa zamani wa kundi la waasi mwenye umri wa miaka 60 imechukuliwa na Nestor Girukwishaka.

Chama cha CNL ambacho kilianzishwa mwaka wa 2019, kilisimamishwa mwaka jana na serikali ya Burundi ikikituhumu kutotii sheria.

Wakosoaji wanasema hatua hiyo ya wizara ya mambo ya ndani ni juhudi za kukandamiza upinzani kabla ya uchaguzi wa bunge wa 2025 na inaweza kuirejesha nchi hiyo kwenye mzozo wa kisiasa.

Katibu mkuu wa chama Simon Bizimungu amelaani kuondolewa kwa Rwasa akisema ni kinyume na katiba ya chama chao.

“Huu ni ukiukaji wa kifungu cha 47 cha sheria za chama ambacho kinasema kwamba ni rais na mwakilishi halali pekee ndiye anaruhusiwa kuitisha mkutano wa aina hiyo,” Bizimungu ameliambia shirika la habari la AFP.

Bizimungu amemshtumu waziri wa mambo ya ndani Martin Ninteretse kwa kukataa kumruhusu Rwasa kuandaa mkutano mkuu wa chama tarehe 2 Machi, lakini “ametoa ruhusa kwa kundi dogo la wapinzani kufanya mkutano haramu na kutupokonya chama.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!