Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Moto Katiba Mpya wachipuka upinzani
Habari za SiasaTangulizi

Moto Katiba Mpya wachipuka upinzani

Rais Jakaya Kikwete (kushoto) na Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein (katikati) wakionesha katiba Mpya
Spread the love

 

KASI ya kutaka Katiba Mpya kabla ya uchaguzi mkuu 2025, imevisukuma vyama vya upinzani kutaka kuungana. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Vyama hivyo vimeeleza kuwa tayari kushirikiana ili kuhakikisha Katiba Mpya inapatikana kabla ya uchaguzi mkuu 2025.

Chama cha ACT-Wazalendo, Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), NNCR-Mageuzi na Chama cha Democratic ni miongoni mwa vyama vilivyoeleza utayari wa kushirikia kufikia lengo hilo.

Wakizungumza kwawakati tofauti na MwanaHALISI Online kwa simu, leo Jumanne tarehe 9 Februari 2021, viongozi wa vyama hivyo wamesema, ili Katiba hiyo ipatikane, wanapaswa kuungana.

Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo ameshauri vyama vya upinzani kutumia Azimio la Zanzibar, lililotolewa na vyama sita mwaka 2018, katika kudai Katiba hiyo.

Amesema, suala la kudai Katiba Mpya sio la vyama vya siasa peke yake, bali ni la watu wote ikiwemo asasi za kiraia, viongozi wa dini na wananchi.

Ado Shaibu, Katibu Mkuu ACT-Wazalendo

Amesema, chama chake kinafanya vikao vya ndani kuangalia njia itakazotumia kudai Katiba hiyo.

“Kiutaratibu ni kwamba, mkishatoka kwenye uchaguzi halafu ukawa na matokeo kama yale, yaliyotokea lazima chama kijifungie ndani kwa muda mrefu ili kutafakari kwa hali ya utulivu wala sio ghadhabu, hasira na jazba.

Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara amesema, chama hicho kimeanza kushirikiana na vyama vingine katika harakati hizo.

Amesema, viongozi wake wa ngazi ya wilaya huwashirikisha viongozi wa vyama vingine katika makongamano ya kudai Katiba Mpya.

“Tumesema kabisa mapema jukumu hilo si la chama kimoja, na sasa hivi viongozi wa wilaya wakifanya makongamano, wanaalika viongozi wa vyama vingine wakionesha ushirikiano,” amesema Sakaya.

Ametoa wito kwa asasi za kiraia na taasisi binafsi kushirikiana na vyama vya siasa katika mapambano hayo.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), aliye pia Mbunge wa Viti Maalum, Magdalena Sakaya

“Kushirikiana na vyama sisi tuko tayari, si vyama tu hata taasisi mbalimbali vyote kwa pamoja jukumu letu ni moja, nia njema kudai Katiba Mpya,” amesema Sakaya.

Abdul Mluya, Katibu Mkuu wa Chama cha Democratic Part (DP) amesema, chama chake kiko tayari kushirikiana na vyama vingine vya upinzani, katika harakati za kudai Katiba Mpya, endapo vitatumia njia za kisheria ikiwemo kwenda mahakamani na si kwa maandamano na fujo.

“Sisi tutadai kwa hoja na kisheria, sisi hatutadai kwa kuandamana na kurusha mawe barabarani, kwa hiyo kama kuungana  maana yake vyama lazima vifanane kiitikadi na namna ya kutengeneza muungano wa kuitafuta hiyo Katiba,” amesema Mluya.

Hashimu Rungwe, Mwenyekiti wa Chaumma Taifa amesema, chama chake kiko tayari kushirikiana katika harakati hizo, kwa kuwa Katiba Mpya ni muhimu kuelekea chaguzi zijazo.

Edward Simbeye, Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma wa NCCR-Mageuzi ameeleza kuwa, vyama ni vya wananchi na wote wana lengo moja.

Edward Sembeye, Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma wa NCCR Mageuzi

“Tutashirikiana nao kudai Katiba Mpya, sababu ni mali ya wananchi ni jambo la kitaifa, kwa hiyo linahitaji utaifa zaidi.

“Juzi tumetoka kwenye kikao cha Kamati Kuu ambacho kimeridhia maamuzi ya kikao cha Halamshauri Kuu, chama kiingie kwenye mchakato wa kudai Katiba Mpya,” amesema.

Amesema, kati ya tarehe 15 na 16 Februari 2021, chama hicho kitakuwa na kikao cha pili cha Kamati Kuu kitakachoamua aina gani ya mfumo watakayotumia kudai Katiba Mpya.

“Malengo yetu kabla ya 2024 kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu, tuwe na Katiba Mpya yenye Tume Huru ya Uchaguzi, tume huru ya uchaguzi itambulike kikatiba,” amesema.

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF Taifa aliibua mjadala wa upatikanaji wa Katiba Mpya na kwamba, chama chake hakitashiriki uchaguzi wowote hadi pale Katiba Mpya yenye Tume Huru ya Uchaguzi itakapopatikana.

Prof. Lipumba alitoa kauli hiyo mwishoni mwa mwaka jana wakati akilalamikia matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.

Baadaye baadhi ya wanasiasa wa upinzani akiwemo Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia walisema, chama chake kitaanzisha vuguvugu la kudai Katiba Mpya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!