May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nape: Biashara zinafungwa, kodi kubwa

Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama (CCM)

Spread the love

 

KIWANGO kikubwa cha kodi kwa wafanyabiashara, kimesababisha biasharanyingi kufungwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama (CCM) leo Jumanne tarehe 9 Februari 2021, bungeni mjini Dodoma.

“Ni kweli tunafurahia kukusanya kodi lakini matokeo tunayo furahia ni ya muda mfupi sana, sababu idadi ya biashara zinazofungwa ni nyingi mno. Kesho hatuna ng’ombe wa kumkamua maziwa,” amesema Nape.

Akifafanua kuhusu suala hilo, amesema kinachochangia biashara hizo kufungwa, ni hatua ya serikali kutumia kikosi kazi binafsi katika kukusanya mapato kutoka kwa wafanyabishara, na kuacha kutumia wataalamu wa ukusanyaji kodi.

“Kuna changamoto kubwa sana inaendelea katika nchi yetu, ukusanyaji kodi ni taaluma, changamoto tuliyonayo tumemua kuacha kuwatumia wataaluma ambayo ndio wakusanya kodi, tumeamua kutumia tax forces (kikosi maalumu) kukusanya kodi.

“Tax forces sababu sio taaluma yao, wanachofanya wanakwenda kuuwa biashara, kelele hizo zote tunazosikia ni kwa sababu tumeamua kuacha kutumia taaluma ya ukusanyaji kodi. Tumeamua kutumia task force kukusuanya kodi, sababu sio taluma yao wanachoangalia ni kufikia lengo walilopewa,” amesema.

Amesema, vikosi kazi hivyo vinavyoundwa kukusanya kodi, hukusanya kodi bila kuangalia hali ya kiuchumi ya mfanyabiashara.

“Sasa kinachotokea ni kwamba wanakwenda kwa mfanyabiashara na hawajali maisha yake ya kesho, hawajali kwamba wanatakiwa kukusuanya kodi leo,  wamuachie uwezo wa kuzalisha ili wakusanye na kesho, tunafurahia matokeo ya muda mfupi,” amesema Nape.

Kufuatia changamoto hiyo, Nape ameishauri serikali ipunguze kutumia vikosi kazi maalumu katika ukusanyaji kodi, badala yake itumie wataalamu kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ili kunusuru biashara zisifungwe.

“TRA imeanzishwa kufanya kazi hiyo, nao hao wamesomea, tukijiwekeza kwenye task force hatutakuwa na cha kukusanya sababu sio kazi yao.

“Nimeambiwa baadhi ya maeneo wanakwenda tayari na draft (maelezo) ya kesi za uhujumu uchumi, wanawatisha watu, inabidi watoe fedha, wakitoa fedha watu wanafunga biashara zao, muendelezo huu wa tunachokifanya mwisho wake utakuwa nini?” amehoji.

error: Content is protected !!