May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jeshi la watu 44 Simba lapaa kwenda Congo

Spread the love

 

MSAFARA wa watu 44, wakiwemo wachezaji, viongozi na benchi la ufundi la klabu ya Simba umeondoka jijini Dar es Salaam hii leo kuelekea nchini Jamhuri ya Demokrasia Congo kupitia Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya AS Vita Club. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam …(endelea).

Simba ambayo kwa sasa ipo hatua ya makundi itatupa karata yake ya kwanza kwenye kundi A, dhidi ya AS Vita Club kwenye mchezo utakaopigwa nchini Congo DR, siku ya Ijumaa tarehe 12 Februari 2021.

Kwa mujibu wa Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema, msafara huo umejumuisha jumla ya wachezaji 26, viongozi tisa pamoja na watu tisa wa benchi la ufundi.

Simba imeondoka majira ya saa 10:45 jioni kwenye Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere na Shirika la Ndege la Ethiopia, ambapo watafika Addis Ababa majira ya saa 1:25 usiku, na kesho Juamtano wataondoka Ethiopia majira ya saa 4 asubuhi na kuwasili Kinshasa majira ya saa 6:10 mchana.

Wachezaji pekee wa klabu hiyo ambao hawakusafiri na timu hiyo ni nahodha wao, John Bocco anayesumbuliwa na majeruhi sambamba na kiungo mshambuliaji Perfect Chikwende ambaye kanuni hazimruhusu kucheza michuano hiyo.

Kwenye michuano hiyo Simba ipo kundi A, sambamba na mabingwa watetezi wa kombe hilo timu ya Al Ahly kutoka Misri, El Merriekh ya Sudan na AS Vita Cluc ya Congo DR.

error: Content is protected !!