May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba, Yanga zapangwa na ligi daraja la kwanza kombe la FA

Spread the love

 

DROO ya hatua ya 32 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (FA) imechezeshwa hii leo ambapo jumla ya michezo 16 itachezwa kumsaka bingwa kwa msimu wa 2020/21. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa upande wa mabingwa watetezi wa kombe hilo klabu ya Simba wataanza kampeni yao kwa kuwavaa African Lyon inayoshiriki ligi daraja la kwanza ambao watakuwa nyumbani, huku watani zao klabu ya Yanga wataawalika Kengold kutoka ligi daraja la kwanza kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Uchezeshwaji wa droo hiyo umefanyika hii leo tarehe 9 Februari 2021, kwenye makao makuu ya Azam TV yaliyopo Tabata, jijini Dar es Salaam na michezo hiyo itaanza kupigwa kuanzia Machi mwaka huu.

Ratiba kamili hapo chini

error: Content is protected !!