JOHN Mnyika, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania, ametaja sababu zilizomsukuma kutogombea Ubunge wa Jimbo la Kibamba, katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).
Mnyika ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Kibamba anayemaliza muda wake (2015 hadi 2020) , amekuwa mbunge katika vipindi viwiili mfululizo, ambapo kipindi cha kwanza alikuwa Mbunge wa Ubungo mwaka 2010 hadi 2015.
Katika kura za maoni za jimbo hilo zilizofanyika jana Jumanne, Mnyika hakuwa sehemu ya waliotia nia kwa kuchukua fomu na kurejea. Ernest Mgawe, ndiye alishika kwa kupa kura 30 kati ya 71 za wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo.
Wengine waliofuata nyuma ya Mgawe, ni Nemes Tarimo aliyepata kura 22 na Humphrey Sambo, ambaye alikuwa diwani wa Mbezi, aliyeambulia kura 19.
Soma zaidi hapa
John Mnyika akimbia ubunge Kibamba
Kupitia akaunti yake ya Twitter, Mnyika amezungumzia hatua yay eye kukaa kando kwenye mbio za kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020.
Katibu Mkuu huyo wa Chadema amesema, hata Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere alijiuzulu Uwaziri Mkuu wa Serikali ya Tanganyika, kwa ajili ya kukijenga Chama cha TANU.
Hata hivyo, Mnyika amesema uamuzi wa kutogombea tena aliutoa kabla ya kuteuliwa na Mkutano Mkuu wa Chadema kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Desemba mwaka 2019.
“Haya nilisema kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu mwezi Desemba 2019, Nyerere aliwahi kuachia Uwaziri Mkuu akabaki kuimarisha TANU, nami sitagombea Ubunge 2020 nitumikie ipasavyo ukatibu mkuu wa Chadema.
Tushinde chaguzi tulete mabadiliko,” ameandika Mnyika katika ukurasa wake wa Twitter.
Haya nilisema kabla ya kuteuliwa kuwa KM Dec 2019: https://t.co/wrF6WPG4Hy . Nyerere aliwahi kuachia uwaziri mkuu akabaki kuimarisha TANU, nami sitagombea ubunge 2020 nitumikie ipasavyo ukatibu mkuu @ChademaTz tushinde chaguzi tulete mabadiliko nchini.
— MNYIKA John John (@jjmnyika) July 14, 2020
Kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, tarehe 19 Desemba 2019 mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa Chadema, Mnyika alisema anauweka rehani ubunge wake, ili aongeze nguvu katika mapambano ya kuitoa Serikali ya CCM madarakani.
“Nikiwa naenda jimboni kamati tendaji wananiambia tunakusikia uko huko na huko na nilikuwa nawaambia viongozi wenzangu na wananchi kwenye mikutano, tulishinda ubunge mara mbili na halmashauri, kwa muundo wa katiba mbovu inayoongoza nchi yetu, madaraka makubwa ya nchi yamewekwa mikononi mwa rais,” alisema Mnyika
“Kulikuwa na tatizo kwenye urais kunakuwa na tatizo kwenye bunge, matokeo yake hata ukiwa na madiwani wachache huwezi kufanya mabadiliko ya kutosha na suluhusisho pekee ni kuiondoa serikali na kuweka sera mpya,” alisema
Mnyika alisema, “nikawaambia nyakati zote wenzetu wa Kibamba kwa kazi ya kuiondoa CCM madarakani afadhali niweke rehani ubunge wa jimbo moja kwa manufaa ya kuletea maendeleo Watanzania kwa kuitoa serikali ya CCM madarakani.”
Leave a comment