Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Ubunge CCM: 2020 Shuguli pevu
Habari za SiasaTangulizi

Ubunge CCM: 2020 Shuguli pevu

Spread the love

NDANI ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuna shughuli pevu katika hatua ya upigaji kura za maoni ili kupata wateule wa ubunge kwenye majimbo mablimbali nchini. Anaandika Mwandishi Wetu…(endelea).

Ni baada ya majina ya wanasiasa wakongwe ‘waliosahaulika,’ wafanyabiashara, wahadhiri, wanahabari na hata wale walioukwaa uwaziri baada ya kuteuliwa ubunge na Rais John Magufuli kuwania nafasi hiyo.

Baadhi ya majina yaliyojitokeza kwenye uchuaji fomu, yameacha

Soma zaidi hapa

Mwandishi Azm Tv ajitosa Ubunge Kigoma mjini 

fadhaha, mshangao na hata butwaa kutokana na pengine kutotarajiwa, zaidi ni majina ya wanasiasa ‘waliosahaulika,’ wasanii, waandishi pia waliounda juhudi wakitokea vyama vya upinzani.

CCM imefungua pazia la uchukaji fomu jana tarehe 14 Julai 2020, zoezi hilo linatarajiwa kukoma tarehe 17 Julai 2020. Ili kuweka rekodi sawa, MwanaHALISI Online linakuletea miongoni mwa majina ya makada wa chama hicho ambao wamechukua fomu tarehe 14 Julai 2020.

Soma zaidi hapa

Makonda kujitosa Ubunge, mjadala waibuka

Peter Lijualikali, huyu alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kilimanjaro (Chadema), alihama chama hicho na kujiunga na CCM. Tayari amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa ili atetea kiti hicho kupitia chama hicho.

David Silinde, alikuwa Mbunge wa Jimbo la Momba (Chadema), kile kilichoitwa mgogoro na chama chake cha awali kilimsukuma na kugamia CCM, safari hii ametoka Momba na kwenda kuomba kuteuliwa na CCM kugombea Jimbo la Tunduma, Mbeya.

Kalist Lazaro aliyekuwa Meya wa Jiji la Arusha (Chadema), alijiuzulu na kukimbilia CCM, tayari amechukua fomu ya kutaka jimbo la Arusha Mjini. Lema ameanza kuongoza jimbo hilo tangu mwaka 2010.

Soma zaidi hapa

Ubunge Ccm: Angellah Akilimali ajitosa Ukonga

Kijana Mrisho Gambo, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha amechukua likizo ili kumng’oa Lema, tayari mkoa huo kwa sasa hauna mkuu wa mkuoa kwa kuwa Gambo amechukua fomu ya kuwania jimbo hilo.

Aggrey Mwanri, mzee wa ‘sukuma ndani’ ama ‘soma iyoooo,’ kabla ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge kwenye jimbo la Siha, alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora. Mwari baada ya kukosa ubunge mwaka 2015, amerejea Siha kuomba ridhaa ya chama chake.

Soma zaidi hapa

Waziri Mkuu Tanzania achukua, arejesha fomu Ruangwa

Uamuzi wa Prof. Juma Athumani Kapuya, mwanasiasa huyo mkongwe na waziri wa zamani kuchukua fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo la Kaliua, Tabora umeshtua wengi, si kwamba hafai la! Ni mwanasiasa aliyesahaulika kwenye medani za siasa.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Kitivo cha Sheria, Dk. James Jesse amejitosa Jimbo la Segerea huku Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akichukua fomu Jimbo la Kawe linaloongozwa na Halima Mdee wa Chadema.

Haikuwa rahisi kudhani bosi wa zamani wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei angeweka jina lake katika orodha ya watia nia kwenye Jimbo la Vunjo, Kilimanjaro Dk. Kimei anataka kumng’oa James Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa NCCR-Magezi.

Jimbo la Mbozi linatolewa udenda na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye, anakwenda kumenyana na Silinde aliyekimbia Chadema na kuhamia CCM.

Fredrick Lowassa, mtoto wa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa anatafuta ridhaa ya CCM kimpitishe kuwania ubunge katika Jimbo la Monduli. Ndani ya jimbo hilo, baada ya Fred kuchukua fomu, waliotia nia wengine wanajiuliza, itakuwaje?’

Ni kwa kuwa, jimbo hilo lilikuwa likiongozwa kwa zaidi ya miaka 20 na baba yake Lowassa, tayari Lowassa amerejea CCM na yupo bega kwa bega na Rais Magufuli. Mbunge anayemaliza muda wake kwenye jimbo hilo, naye anasubiri hukumu ya kura za maoni.

Aliyekuwa Diwani wa Hananasif, Abbas Tarimba yeye amechukua fomu kuwania ubunge jimbo la Kinondoni. Tarimba alikuwa Mwenyekiti w Kalabu ya Yanga.

Waandishi wa habari nao hawako nyuma, kwenye mbio hizo za kuwani uwakilishi wa wananchi.

Mtia nia aliyechafua mitandao ya kijamii baada kujitokeza ni aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Francis Nanai.

Ni kwa kuwa, akiwa mkurugenzi baadhi ya waandishi waling’olewa kwenye taasisi hiyo baada ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii kile walichoamini ni haki yao kuhusu utawala wa Rais Magufuli, Rais Magufuli ni mwenyekiti wa Nanai.

Mwandishi wa habari, Dk. Tumain Msowoya, yeye amechukua fomu kuwania ubunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa kupitia kundi la Umoja wa Wanawake Tanzania wa chama hicho.

Mtangazaji wa Clouds Media, Harris Kapiga amejitosa Jimbo la Singida Mashariki lililokuwa likiongozwa na Tundu Lissu (Chadema), baada ya Lissu jimbo hilo ‘alipewa’ Miraji Mtaturu wa CCM.

Mwandishi mwingine wa habari, Dotto Kahindi anaomba huruma ya CCM kumwachia Jimbo la Busanda mkoani Geita. Lolensia Bukwimba (CCM) ndiye anayemaliza muda wake.

Idda Mushi wa ITV, ameomba kupitishwa na chama hicho, agombee Jimbo la Moshi Vijijini huku Mkurugenzi wa Gazeti la SAUTI HURU, Albert Kawogo akichukåua fomu Jimbo la Bagamoyo mkoani Pwani.

Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika la Bunge la Tanzania, alikuwa Mbunge wa Kuteuliwa na Rais Magufuli, safari hii ameamua kwenda kupambana kwenye Jimbo la Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Mbeya Mjini (Chadema).

Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria alikuwa mbunge wa kuteuliwa, safari hii amerudi nyumbani Kilosa kuomba kuteuliwa kusimamia jimbo hilo. Jimbo hilo linaoongozwa na mwana CCM mwenzake Baraka Bawazir.

Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango, anawaomba wana CCM wa Buhingwe wamchague. Jimbo hilo linaongozwa na Albert Obama wa CCM.

Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo amechukua fomu Jimbo la Kasulu Mjini linaloongozwa na Daniel Nswanzugwako wa CCM.

Mchuano katika majimbo hayo ya Buhingwe na Kasulu Mjini, ulianzia ndani ya Bunge lililohitimishwa Juni 16 mwaka huu, kwa Profesa Ndalichako kutangaza kuwania jimbo la Nswanzugwako ambaye naye alimkaribisha.

Hali hiyo ilikuwa kati ya Obama aliyesema wana Buhingwe wanajua wametoka wapi, wapo wapi na wanakwenda wapi huku Dk. Mpango akisema wakimpendeza wana Buhingwe wamchague yeye.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!