October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ubunge CCM: 241 wajitosa majimbo tisa K’njaro

Mkurugenzi wa Ibraline Foundation , Ibrahim Shayo akiingia kwenye gari mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Moshi mjini katika ofisi za Chama cha Mapinduzi(CCM)

Spread the love

WANACHAMA 241 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania, wamejitokeza kuchukua fomu kuomba kuteuliwa kugombea ubunge katika majimbo tisa mkoani humo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro…(endelea)

Wanachama hao 241 walijitokeza jana Jumanne tarehe 14 Julai 2020 katika siku ya kwanza ya uchukuaji fomu hizo katika ofisi za wilaya za CCM.

Ratiba ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu za udiwani, ubunge na uwakilishi ndani ya CCM utahitimishwa tarehe 17 Julai 2020 ili kuruhusu michakato mingine ya kuwapata wagombea.

Akizungumza na vyombo vya habari mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya, Katibu wa CCM wa mkoa huo alisema, kati ya wagombea hao 241, wanawake ni 27 na wanaume 214.

Soma zaidi hapa

Ccm wafurika kuchukua fomu za ubunge moshi mjini

Akifafanua mchanganuo wa wagombea hao, Mabihya alisema, Kjimbo la Moshi Mjini ni 14, Siha 21, Mwanga 31, Hai 25, Moshi Vijijini 35, Vunjo 28, Same Magharibi 28, Same Mashariki 24 na Rombo 35.

”Nitoe wito kwa wanaCCM wote waliojitokeza, watumie haki yao ya kikatiba ambayo ni ya kuchagua na kuchaguliwa lakini pia nawahakikishia kwamba uchaguzi ni uhuru na haki utakaozingatia katiba ya chama chetu ili tupate miongoni mwao atakaye peperusha bendera ya chama,” alisema Mabihya

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari zaidi

error: Content is protected !!