KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika amesema kupungua kwa idadi ya wapiga kura katika uchaguzi kumetokana na watu kupoteza imani na mifumo ya uchaguzi. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).
Mnyika ameyasema hayo leo tarehe 11 Machi 2024, jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa wadau wa siasa ulioratibiwa na Kituo cha Demokrasia nchini (TCD).
“Sisi kwa tathmini yetu tunaona idadi ya wapiga kura inapungua kwa sababu watu wamepoteza imani na mifumo ya uchaguzi” amesema Mnyika.
Mnyika amesema serikali ingeweza kuirejesha imani kwa Watanzania kwa kupeleka miswada mizuri ya mabadiliko ya sheria za vya vyama vya siasa.
“Kupelekwa miswada bungeni kungeweza kujenga imani lakini bahati mbaya kumepelekwa miswada mibovu pia karibu na uchaguzi wa serikali za mitaa” amesema Mnyika.
Amesema kuwa ili watu wawe na imani na idadi ya wapiga kura iongozeke.
“Tukitaka kuongeza idadi ya wapiga kura lazima tuongeze imani katika mifumo ya uchaguzi, lazima tudai Katiba mpya, marekebisho ya kisheria, tutengeneze uwanja sawa wa uchaguzi” amesema Mnyika.
Leave a comment