Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mitumbwi 2 yazama Ziwa Victoria, 14 wafariki dunia
Habari MchanganyikoTangulizi

Mitumbwi 2 yazama Ziwa Victoria, 14 wafariki dunia

Spread the love

WAUMINI 14 wa Kanisa la KTMK, Kijiji cha Ichigondo, wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, wamefariki dunia, huku 14 wakijeruhiwa baada ya mitumbwi waliyokuwa wamepanda kuzama ndani ya Ziwa Victoria. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu, tarehe 31 Julai 2023 na Jeshi la Polisi Mkoani Mara, tukio hilo limetokea jana jioni, wakati waumini hao wakitoka ibadani kuelekea kijijini kwao Bulomba.

Taarifa za awali za Jeshi la Polisi zinadai kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni mitumbwi kupigwa na dhoruba kali.

“Hizo taarifa za kweli, kwa sasa tupo kwenye eneo la tukio taarifa kamili hazijakamilika tutazitoa baadae. Lakini taarifa zilizopo sasa watu 14 wamepoteza maisha,” amesema msaidizi wa Kamanda wa Polisi Mara, Salum Morcase, akizungumza na MwanaHALISI Online kwa simu.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dk. Vicent Naano, amesema zoezi la uokoaji miili linaendelea ambapo hadi sasa mwili wa mtoto mchanga umeshaokolewa kutoka ziwani.

Chama cha Wananchi (CUF), kupitia Mkurugenzi wake wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, Mhandisi Mohamed Ngulangwa, kimetoa salamu za rambirambi kufuatia vifo hivyo.

“Tunawaombea wale wote waliopoteza maisha kutokana na ajali hii mbaya, wapate mafikio mema. CUF kinatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu mzito na tunawaombea subira na uvumilivu katika wakati huu mgumu. Tunatoa wito kwa Serikali kuimarisha huduma ya uokoaji na uopoaji zitokeapo ajali za majini,” imesema taarifa ya Mhandisi Ngulangwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

Habari Mchanganyiko

GGML yaja na teknolojia za kisasa maonesho ya OSHA Arusha

Spread the loveKATIKA kuelimisha wananchi na washiriki wa maonesho ya usalama na...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!