Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Makamba: ‘Madalali’ nifuateni mimi, iacheni Tanesco
Habari za SiasaTangulizi

Makamba: ‘Madalali’ nifuateni mimi, iacheni Tanesco

Waziri wa Nishati, January Makamba
Spread the love

WAZIRI wa Nishati, January Makamba amewataka watu wasiingize siasa katika utendaji wa wizara yake, kwa kuwa kitendo hicho kinaathiri maendeleo ya nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Makamba ametoa wito huo leo Jumatatu, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa taarifa ya mwaka wa fedha 2021/22, jijini Dar es Salaam.

“Siasa tuweke pembeni kidogo, kwenye haya mambo ya muhimu ya kusimamia mradi wa Bwawa la Julius Nyerere, gridi imara, umeme vitongojini ni mambo makubwa. Tunaosimamia siasa hatuwezi kuitenganisha, lakini mimi nataka hawa mabwana wa TANESCO msiwaingize kwenye mambo yetu ya siasa,” amesema Makamba.

Makamba amesema “nyie wanasiasa njooni kwangu, hawa mabwana waachwe kwa sababu sisi tunawezana tusiwaangize hawa ni mafundi wanafanya shughuli zao.”

Waziri huyo amedai kuwa, kuna baadhi ya wanasiasa na madalali wao wanarusha tuhuma dhidi ya wizara yake pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kitendo alichodai kinavuruga utendaji wa taasisi hiyo.

“Mkurugenzi wa TANESCO (Maharage Chande) anasema wanahangaika wanasema nina majenereta Karikaoo…tunataka wafanyakazi wa TANESCO na bodi wafanye kazi kwa utulivu. Tuwaombe wanasiasa wenzangu au madalali wao nifuateni mimi, msiwafuate hawa mabwana ili wafanye kazi zao vizuri,” amesema Makamba.

 

Makamba ametoa kauli katika kipindi ambacho kumeibuka tuhuma mitandaoni dhidi ya wizara yake, akidaiwa kuiongoza vibaya katika maeneo mbalimbali, hususan usambazaji umeme na uingizaji mafuta nchini.

Makamba amesema hata kama wizara yake itazongwa lakini haitaacha kusema ukweli kwa wananchi juu ya utekelezaji miradi mbalimbali inayoendelea nchini.

“Tulisema tangu mwanzo kwenye masuala ya umeme hatutadanganya watu, wacha tupigwe mishale, tuzongwe zongwe lakini ili tuwe huru na tufanye kazi tukiwa tumelala usingizi hatuwezi kusema hakuna mgawo wakati unakaribia,” amesema Makamba na kuongeza”

“Hatuwezi kutoa sababu za uongo kuhusu changamoto, tutasema wazi sababu ni shirika la umma tunao wajibu huo. Hatuogopi hukumu kwa mambo ambayo changamoto zake zinajulikana na utatuzi wake unafanyiwa kazi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!