Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Makamba awataka Watanzania kuvumilia machungu ya mageuzi Tanesco
Tangulizi

Makamba awataka Watanzania kuvumilia machungu ya mageuzi Tanesco

Spread the love

WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba amewataka wananchi wawe na subira wakati Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linafanya mageuzi ya utendaji kazi wake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Makamba ametoa wito huo leo tarehe 31 Julai 2023, jijini Dar es Salaam, akizungumzia mpango mkakati wa miaka 10 wa shirika hilo.

“Ambacho sisi tunawaomba watanzania na wadau wote ni subira, mtupe muda sababu mabadiliko yanachukua muda mrefu, mabadiliko ni magumu na machungu sababu yanakwenda kinyume na utaratibu tuliozoea. Mabadiliko yanayofanyika yanaweza yasieleweke mwanzoni,” amesema Makamba.

 

Makamba ametoa mfano wa mabadiliko yanayotaka kufanywa na TANESCO yaliyozua mjadala, ya kuipa kampuni binafsi tenda ya kushughulika huduma kwa wateja “kulikuwa na mjadala mkubwa sana kituo cha kutoa huduma inakuwaje mmepa mtu binafsi awapokelee simu zetu, lakini ukiangalia tuna kampuni za simu zinapokelewa.”

Waziri huyo amesema Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuipa mtaji TANESCO ili itekeleze mipango yake kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wananchi na Afrika kwa ujumla.

“TANESCO ni shirika ambalo ukilipa Dola za Marekani 5 bilioni, linaweza kuzitumia zote wakati wengine ukiwapa Dola 1 bilioni wanahangaika. Lakini sekta ya umeme ni nyeti yenye njaa kubwa ya mtaji, bila mtaji na uwekezaji hizi ni stori kabisa. Bahati nzuri Serikali inajua hivyo na tunafanya juhudi zote kuitafutia mtaji,” amesema Makamba.

Akitaja mafanikio ya TANESCO, Makamba amesema thamani ya mali zake imeongezeka hadi kufikia Sh. 19 trilioni, ambapo imefanikiwa kufungua ofisi nchi nzima.

Amesema TANESCO imefanikiwa kuwaunganishia huduma ya umeme wateja 500,000 ikiwa ni ongezeko la wateja 200,000 kutoka makadirio yake ya kufikisha huduma hiyo kwa wateja 300,000.

Naye Mkurugenzi wa TANESCO, Maharage Chande, amesema shirika hilo linakusudia kuendelea na mipango yake ya kuboresha huduma kwa wateja wake, kupitia miradi mbalimbali ikiwemo wa kufua umeme katika Bwawa la Julius Nyerere, ambao unatarajia kuanza kuzalisha umeme Juni 2024.

“Kupata umeme wa Mwalimu Nyerere ni muhimu katika maendeleo ya nchi yetu na ule umeme kutotosha kwa kipindi fulani tutakuwa tumeondokana na tatizo hilo,” amesema Chande na kuongeza:

“Hii miezi nane mpaka 10 tunayopitia tunajitahidi kuendelea kuwa na ufanisi huku tukisubiri umeme wa bwawa kuingizwa sababu changamoto tunazopitia kipindi hiki tusipokuwa na uvumilivu tunaweza kukata tamaa tukataka kuingia mkataba wa uzalishaji umeme kwa dharura ambao ni ghali.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!