July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Milioni 500 yatengwa kununua vifaa tiba Mufindi

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania imetenga Sh.500 milioni kwa ajili ya kununua vifaa tiba kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. Anaripoti Jemima Samwel DMC … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne, tarehe 18 Mei 2021, katika kipindi cha maswali na majibu, bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Tamisemi, David Lusinde, wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu, Nancy Nyalusi.

“Je, ni Iini Serikali itakamilisha ujenzi na kuanza kutumia Hospitali ya Wilaya ya Mufindi?”

Silinde amesema, katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali imeipatia halmashauri ya wilaya ya Mufindi Sh.500 milioni, kwa ajili ya ujenzi wa wodi tatu za hospitali ya halmashauri.

“Hadi Aprili 2021, ujenzi wa majengo saba ambayo ni jengo la utawala, jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD), jengo la maabara, jengo la mionzi (X-ray), jengo la wazazi na jengo la kuhifadhia dawa,” amesema

“Jengo la kufulia, umekamilika na ujenzi wa wodi ya watoto na wodi ya magonjwa mchanganyiko kwa wanaume na wanawake upo katika hatua ya upandishaji wa ukuta,”amesema Silinde.

David Silinde, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Pia, katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali imetenga Sh.500 milioni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Mufindi.

“Katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali imetenga Sh.800 milioni kwa ajili ya ujenzi wa jengo la upasuaji, jengo la kuhifadhia maiti na wodi ya upasuaji kwa wanaume na wanawake.”

Silinde amesema, “Hospitali ya Wilaya ya Mufindi imeanza kutoa huduma za wagonjwa wa nje na inatarajiwa ifikapo mwishoni mwa mwaka 2022.”

“Hospitali hiyo itaanza kutoa huduma kwa zaidi ya asilimia 90 ya huduma zote zinazotakiwa kutolewa katika ngazi ya Hospitali ya Halmashauri,” amesema Silinde.

error: Content is protected !!