Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Masheikh wa Uamusho: Mahakama kuamua rufaa mashtaka 14
Habari Mchanganyiko

Masheikh wa Uamusho: Mahakama kuamua rufaa mashtaka 14

Spread the love

 

MAHAKAMA ya Rufaa Tanzania, kesho Jumatano, tarehe 19 Mei 2021, inatarajia kutoa uamuzi wa rufaa iliyowasilishwa na Serikali, kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu uliowafutia mashtaka 14 Masheikh wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne tarehe 18 Mei 2021, na Msemaji wa Shura ya Maimamu Tanzania, Ustaadhi Ibrahim Mkondo.

Mkondo amesema, Jopo la Mawakili wa Masheikh hao 23 wanaokabiliwa na makosa ya ugaidi kwenye Makahama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, limetakiwa kufika Mahakama ya Rufaa kesho Jumatano, kwa ajili ya kupata uamuzi huo.

“Kwa mujibu wa Mwanasheria Kiongozi wa Jopo la Mawakili wa Masheikh, Msajili wa Mahakama ya Rufaa amewatumia wito wa kufika mahakamani kesho.”

“Kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa rufaa iliyowasilishwa na upande wa Jamhuri juu ya Hukumu ya Mahakama Kuu iliyofuta mashauri 14, dhidi ya Masheikh,” imesema taarifa ya Mkondo.

Uamuzi wa Mahakama Kuu wa kuwafutia Masheikh hao mashtaka 14, ulitolewa tarehe 23 April 2021 na Jaji Mustapha Ismail, baada ya kupitia hoja za mawakili wa pande zote mbili. Lakini mwanzoni mwa Mei 2021, upande wa Jamhuri uliamua kukata rufaa dhidi yake.

Washtakiwa hao wanadaiwa kati ya Januari 2013 na Juni 2014 walijihusisha na makosa ya ugaidi, kinyume na kifungu cha 27 (c) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.

Masheikh hao walikamatwa 2012 baada ya kutuhumiwa kusababisha vurugu visiwani Zanzibar.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awalilia 17 waliofariki ajalini wakisafirisha maiti

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000

Spread the love  ZAIDI wakazi 2,000 wa kijiji cha Nyamishiga Kata ya...

Habari Mchanganyiko

Baada ya Congo DR, Somalia mbioni kujiunga na EAC

Spread the love  TAIFA la Somalia liko mbioni kuwa mwanachama rasmi wa...

error: Content is protected !!