October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mgombea urais Z’bar anatoka bara? Dk. Bashiru afafanua

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk. Bashiru Ally

Spread the love

HOJA kwamba, mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar, anachaguliwa Tanzania Bara imepingwa na Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa chama hicho. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema, kinachofanyika ni kwamba majina yalilochaguliwa na Wazanzibari wenye ndani ya CCM, kwenda kupitisha kwenye Mkutano Mkuu ambao kwa kawaida hufanyika jijini Dodoma, yalipo makao makuu ya chama hicho.

Dk. Bashiru ametoa kauli hiyo leo Jumatano tarehe 8 Julai 2020, wakati akihojiwa na Kituo cha Uhai Tv, kuhusu malalamiko ya mgombea urais wa  Zanzibar, kuchaguliwa na wajumbe wa Bara.

         Soma zaidi:-

Akijibu hoja hiyo, Dk. Bashiru amesema mgombea urais wa Zanzibar, huchaguliwa na wanachama wa CCM visiwani humo, kisha huthibitishwa na vikao vya chama hicho, pasina kujali wajumbe wake wanatoka Bara au Zanzibar.

“Mchakato wa kupata mgombe urais Zanzibar huanzia uchukuaji fomu, na wanaohusika ni wanachama wa CCM Zanzibar. Kwa mujibu wa sheria, baada ya hapo hatua ya uteuzi huanza, kuanzia vikao vya Halamshauri Kuu, mchakato upo kikatiba na unakidhi matakwa ya Katiba ya CCM na ya nchi,” amesema Dk. Bashiru.

Dk. Bashiru amesema, wenye mamlaka ya kumchagua Rais wa Zanzibar ni Wazanzibar wenyewe, ambao huchagua mtu wanayemtaka katika Uchaguzi Mkuu wa Urais.

“Vyama vya siasa vinateua wagombea, vyama havichagui rais. Rais wa Tanzania huchaguliwa na Watanzania na wa Zanzibar huchaguliwa na Wazanzibari wenyewe, kinachofanyika CCM ni mchakato wa uteuzi si uchaguzi,” amesema Dk. Bashiru.

Hata hivyo, Dk. Bashiru amesema hana sababu za kujadili zaidi mjadala huo, kwa kuwa hautokani na wanachama wa CCM, bali unavumishwa na watu ambao sio wanachama wa chama hicho.

Katibu huyo wa CCM amesema hoja ya mgombea urais wa Zanzibar kuchaguliwa katika vikao vinavyofanyika Dodoma ni vya kibaguzi, na kwamba wanaCCM hawana hulka hiyo.

“Hao sio wanaCCM, CCM wanaamini katika utaifa na umoja, ndani ya CCM kuna wanachama na si Zanzibar au Bara. Kila mwanachama ana haki na wajibu sawa, na kila wanapokaa ni kikao baina ya WanaCCM,” amesema Dk. Bashiru na kuongeza:

“Na kama si WanaCCM wanaotoa malalamiko hayo, sina sababu ya kujadili mawazo yao, na hayawezi kuwepo. Sio tu katiba hairuhusu ubaguzi, lakini pia ndani ya CCM tunakuwa kama wanachama na mambo yetu yanaendeshwa kama WanaCCM.”

error: Content is protected !!