Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Bashiru amzungumzia Maalim Seif Urais Z’bar
Habari za Siasa

Dk. Bashiru amzungumzia Maalim Seif Urais Z’bar

Maalim Seif Sharrif Hamad, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo
Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, yupo mdomoni mwa Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Bashiru ametoa kauli hiyo leo tarehe 8 Julai 2020, wakati akihojiwa na Kituo cha Uhai TV.

Amesema, licha ya kwamba Maalim Seif anagombea urais kupitia ACT-Wazalendo, CCM haitishiki kwa kuwa kimemshinda mara zote alizogombea kuanzia uchaguzi mkuu wa mwaka 1995.

Maalim Seif amegombea urais mara tano visiwani humo (1995, 2000, 2005, 2010, 2015) kupitia Chama cha Wananchi (CUF). Mara zote hizo amekuwa akidai, anashinda lakini ushindi wake unaporwa na CCM.

Tayari Maalim Seif amechukua fomu ili kuomba ridhaa ya chama chake kuteuliwa kugombea urais visiwani humo kupitia ACT-Wazalendo.

          Soma zaidi:-

Akizungumzia hatua hiyo ya Maalim Seif kugombea tena urais wa Zanzibar, Dk. Bashiru amesema, mwanasiasa huyo mkongwe hatoshinda katika uchaguzi huo.

Amesema, historia ya Maalim Seif yake ni kushindwa katika uchaguzi, hivyo na kuwa hilo haliwezi kubadilika kwenye uchaguzi wa mwaka huu akisisitiza, mwaka huu (Maalim Seif) anagombea kupitia chama kipya na kisicho na nguvu.

Dk. Bashiru amesema, sababu hizo zitaifanya CCM kushinda katika uchaguzi wa urais wa Zanzibar, unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2020.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk. Bashiru Ally

“Kwa upande wa Zanzibar, tutakua na mgombea mpya kabisa, lakini wenzetu wanaweza kusimamisha mgombea ambaye amekuwa akishindwa kila mwaka.

“Maalim Seif, yeye ni mzoefu wa kushindwa lakini zamu hii ni mgeni katika chama chake, kwa hiyo leo hii tunashindana na mzoefu wa kushindwa na mgeni katika chama ambacho hakina mtandao,” amesema Dk. Bashiru.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!