Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mgombea uenyekiti ACT-Wazalendo aweka masharti kukubali matokeo
Habari za Siasa

Mgombea uenyekiti ACT-Wazalendo aweka masharti kukubali matokeo

Spread the love

 

HAMAD Masoud Hamad, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo amesema, iwapo uchaguzi wa mwenyekiti wa chama hicho utakuwa huru na haki, akishindwa atakubaki matokeo. Anaripoti Jabir Idrissa, Zanzibar…(endelea).

ACT-Waalendo inafanya uchaguzi wa mwenyekiti tarehe 29 Januari 2022 ili kujaza nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Maalim Seif Sharif Hamad aliyefariki dunia 17 Febrauri 2021, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Tangu shughuli ya uchukuaji na urejeshaji fomu ilipoanza, vigogo wawili wa ACT-Wazalendo wamejitosa kuwania nafasi hiyo ambao ni Hamad na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho-Zanzibar, Juma Duni Haji maarufu Babu Duni.

Leo Alhamisi, tarehe 13 Januari 2022, Ofisi za ACT-Wazalendo, Vuga visiwani humo, Hamad amerejesha fomu zake huku akisema, “uchaguzi ukiwa wa haki na umeendeshwa kwa uhuru kabisa, hata nikipata kura moja tu yangu maana mimi ni mjumbe wa mkutano mkuu, nitampongeza mgombea aliyenishinda, nitamuinua juu na kumkumbatia na nitamuunga mkono.”

Amesema akichaguliwa kuwa mwenyekiti anaahidi kuongoza mageuzi makubwa ya namna ya kuendesha chama huku akisisitiza falsafa yake ya uongozi itakuwa “ushirikiano na maridhiano,” na kwamba atakisuka upya chama ili kitambulike na kukubalika zaidi na umma.

Hamad ambaye amekuwa kiongozi mwandamizi wa muda mrefu katika maisha yake kama mwanasiasa amesema amedhamiria kuongoza kwa weledi hadi serikali mbili zilizo chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ziamini wakati wa kuridhia kuachia madaraka kwa upinzani unaoongozwa na ACT Wazalendo kupitia uchaguzi, umefika.

Hamad ambaye mwaka 2012, alijiuzulu uwaziri wa mawasiliano na miundombinu Zanzibar kuonesha uwajibikaji kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya MV Spice Islander II na kupoteza mamia ya wananchi waliosafiria kwenda Pemba kutoka Bandari Kuu ya Malindi, amerudisha fomu siku tano baada ya Juma Duni Haji kufanya hivyo.

Nafasi hiyo ya makamo mwenyekiti mpaka sasa wamejitokeza wanachama wawili akiwemo Othman Masoud Othman ambaye kwa sasa ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar akishika nafasi hiyo baada ya Maalim Seif kufariki.

Mwanachama mwengine aliyechukua fomu ya kugombea umakamu mwenyekiti ni Juma Sanani ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya chama. Muda wa mwisho kurudisha fomu za kuomba uteuzi ni tarehe 17 Januari 2022.

Written by
Jabir Idrissa

+255 774 226248

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!