Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari Kesi ya Mbowe: Miamala inayodaiwa ya Rais Mwinyi yaibuliwa
Habari

Kesi ya Mbowe: Miamala inayodaiwa ya Rais Mwinyi yaibuliwa

Dk. HUssein Mwinyi, Rais wa Zanzibar
Spread the love

 

UPANDE wa utetezi, katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, umehoji kwa nini Meneja wa Kitengo cha Sheria cha Kampuni ya Mawasiliano ya Airtell Tanzania PLC, Gladys Fimbari, hakuorodhesha baadhi ya taarifa za miamala ya fedha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Ni katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam ambapo Mbowe na wenzake, Adam Kasekwa, Halfani Bwire na Mohamed Ling’wenya wanakabiliwa na tuhuma hizo za ugaidi.

Fimbari aliulizwa swali hilo leo Alhamisi, tarehe 13 Januari 2022 na Wakili wa utetezi John Mallya, baada ya kuwasilisha mahakamani hapo taarifa za usajili na miamala ya fedha ya namba za simu, 0782237913, 0787555200 na 0784779944, inayodaiwa kufanyika kati ya tarehe 1 Juni hadi 31 Julai 2020, zilizoombwa na Kitengo cha Uchunguzi wa Kisayansi cha Jeshi la Polisi.

Kwa mujibu wa ushahidi wa Fimbari, namba 0784779944, inadaiwa kumilikiwa na Freeman Aikael Mbowe, 0782237913 inamilikiwa na Halfan Bwire Hassan na 0787555200 ni ya Dennis Urio.

Wakili Mallya alimhoji Fimbari akidai, kwa nini hajaleta mahakamani hapo taarifa za miamala zinazodaiwa kufanyika kati ya Hassan na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, akiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Pamoja na miamala ya ACP Ramadhan Kingai, ambaye kwa sasa ni Kamanda wa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Dar es Salaam.

Mahojiano yao yalikuwa kama ifuatavyo;

Mallya: Miamala ya fedha imeombwa kwa hizo namba tatu, imeombwa miamala yake ya kifedha, wewe Polisi umepeleka taarifa ya miamala mingapi?

Shahidi: Kwa namba mbili

Mallya: Kilichokufanya muachie hiyo moja ni nini?

Shahidi: Nilipitiwa

Mallya: Ulipitiwa shahidi, mimi siamini kwamba ni overcite na nitakuuliza maswali kwa nini siamini. Muamala wa mwisho kwenye kielelezo P20 wa tarehe 30 Julai 2020 tusomee?

Shahidi: Kama nimekuelewa vizuri una involve Sh.80,000

Mallya: Namba iliyotumia hiyo fedha ni moja ya namba uliyoombwa utoe miamala ya fedha?

Shahidi: Ni sahihi

Mallya: Hizo fedha Bwire alimtumia Kingai, ungeleta transaction za Bwire tungeona kwa nini hujaleta kuziba ugaidi wa Kingai na watu wengine?

Kwa nini hujaleta such a very important information umeombwa kwenye barua ya Polisi, ukaenda kwenye mtandao uka-print lakini ulivyoona Kingai na watu wa Serikali ukaweka kando kwa nini? Hiyo doubt ataijibu nani kama si wewe?

Shahidi: Bado nasimamia jibu nilililosema, nimepitiwa

Mallya: Kwenye transction za Bwire unasema kuna kupitiwa, kama kuna zingine tutajua.

Kwenye transaction za Bwire kati ya Juni mpaka Julai 2020 umeombwa, kuna miamala ya Waziri wa Ulinzi, sasa hivi ni Rais Mwinyi, alikuwa anamtumia pesa Bwire, sababu aliwahi kufanya kazi jeshini, haya mahusiano tutayaonaje kwenye kupitiwa kote?

Kifuatia maswali hayo, Jaji Joachim Tiganga alimuuliza Wakili Mallya hizo taarifa anazitoa wapi, ambapo mahojiano yao yalikuwa kama ifuatavyo;

Jaji:Hizo information unazitoa wapi?

Mallya: Kutoka kwa mteja wangu akihoji kwa nini Airtell wanaficha

Jaji: Ilikuwa chini ya kiapo?

Mallya: Hapana, lakini wateja wetu wanatupatia taarifa za kesi yao kila siku

Jaji: Nafikiri si vyema kutaja watu wasiokuwepo mahakamani, au mnampango wa kumuita Rais Hussein Mwinyi. Mwinyi atapata nafasi ya kuja hapa?

Mallya: Off couse hatuzuiwii kumuita kama shahidi wetu, anaweza sema Mallya hukusema kweli

Jaji: Mimi nahisi mjikite kwenye yale mambo ambayo tunaweza thibitisha, watu ambao sio subject ya proceedings hizi sio sawa sababu wanaweza wasipate nafasi ya kuja kujitetea mahakamani.

Baada ya Jaji Tiganga kutoa amri hiyo, Wakili Mallya aliendelea kumhoji Fimbari kama ifuatavyo;

Mallya: Shahidi wewe ni wakili, mwansheria mbobezi meneja wa kampuni kubwa ya simu Tanzania, kupitiwa kwako umesema mahakamni ulipitiwa, kupitiwa kwako ni nani atakayekuja kui-cover?

Shahidi: Sifahamu

Jaji Tiganga ameahirisha kesi hiyo hadi kesho Ijumaa, tarehe 14 Januari 2022, ambapo shahidi huyo ataendelea kutoa ushahidi wake kwa kuulizwa maswali ya dodoso na mawakili wa utetezi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!