Monday , 4 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mgogoro wa Spika Ndugai, Prof. Assad watua kwa JPM  
Habari za SiasaTangulizi

Mgogoro wa Spika Ndugai, Prof. Assad watua kwa JPM  

Spread the love

JOB Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania amefikisha kiaina mgogoro unaovuma kwa sasa kati yake na Prof. Mussa Assad, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Rais John Magufuli. Anaripoti Yusuph Katimba … (endelea).

Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya mfumo wa kusimamia uwazi katika mawasiliano ya simu (TTMS) leo Ijumaa tarehe 18 Januari 2018 katika viwanja vya Makao Makuu ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Spika Ndugai amesema, Bunge linafanya kazi vizuri na sio dhaifu.

Spika Ndugai alitoa kauli hiyo mbele ya Rais Magufuli wakati akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo ameeleza namna Bunge lilivyofanya kazi yake na kuwa, matokeo yake ndio kupatikana kwa mfumo huo (TTMS).

Amesema, jambo hili lilianzia bungeni, kulikuwa na mjadala mkubwa…wabunge walitaka kujua kwanini kodi kutoka kwenye Kampuni za Mawasiliano ya Simu ni ndogo.

“Kwa sababu walikuwa wanaagalia nchi ndogo yenye watumiaji wachache kulinganisha na sisi, lakini mapato ya serikali yao yalikuwa makubwa mara kadhaa kuliko sisi Watanzania,” amesema Spika Nduga.

Amesema, ilifika hatua Bunge likalazimika kutengeneza sharia. “Ulipoingia madarakani (Rais Magufuli) ulisema unataka jambo hili lirudishwe bungeni, tukafanya kazi na ukasaini mara moja, leo tunashuhudia hapa mafanikio.

“…hii ndio kazi iliyoanzia bungeni. Bunge limefanywa vizuri na kudhibitisha kuwa bunge letu sio dhaifu.”

SpikaNdugai amesema, bila uthubutu wa Rais Magufuli jambo hili lisingewezekana na kwamba, mtu asiyeelewa anaweza kudhani ni kitu kidogo.

Kumekuwepo na vuta nikuvute kati ya Spika Ndugai, Prof. Assad, wanasheria na wanaharakati mbalimbali baada kutolewa amri kwa Prof. Assad kufika mbele ya Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge ili kuhojiwa juu ya kauli yake aliyoitoa akiwa Marekani.

Prof. Assad alipokuwa Marekani wiki iliyopita katika mahojiano yake na Kituo cha Idhaa ya Kiswahili cha Umoja wa Mataifa alisema kuwa, Bunge ni dhaifu kwa kuwa, linashindwa kusimamia baadhi ya mambo. Kauli hii ‘dhaifu’ imemkera Spika Ndugai na kumtaka afike mbele ya kamati hiyo kujieleza.

Hata hivyo jana Prof. Assad alisema, “neon udhaifu ni lugha ya kawaida sana kwa wakaguzi wanapotoa maoni. Hivyo hakuna kokote ambako nimedhalilisha Bunge.”

Kwenye hafla hiyo Spika Ndugai amemsifu Rais Magufuli kutokana na uimara wake wa kusimamia dhamira yake na hata kufikia mafanikio ya kutengenza mfumo huu.

Kwenye hafla hiyo Spika Ndugai amesema mkuwa, kuna watu wanapenda giza kwa kuwa huwasaidia kupata wanachokipata kwa njia isiyo ya halali na kwamba, huu mfumo (TTMS) ndio mwanga ambao wengi tena wale wakubwa wasingeupenda kwa kuwa, panapomulikwa giza linaondoka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwinyi aungana na Samia kuuaga mwili wa baba yake

Spread the loveRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mtoto wa Mzee Mwinyi amwaga machozi

Spread the loveMtoto wa Hayati mzee Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi ameshindwa...

Habari za SiasaTangulizi

Mzee mwinyi alikuwa mwanademokrasia wa kweli

Spread the loveMtoto wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Mwinyi alikuwa maktaba inayotembea

Spread the loveRais Samia Suluhu hassan amesema Hayati rais mstaafu, Ali Hassan...

error: Content is protected !!