March 2, 2021

Uhuru hauna Mipaka

AU waitaka DR Congo kusitisha kutangaza matokeo

Felix Tshisekedi, Rais wa DR Congo

Spread the love

JAMHURI ya Kidemokrasia ya Congo imetakiwa kuahirisha utangazaji wa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Wito huo umetolewa na Muungano wa Afrika (AU), ambao umoja huo umeonesha kutoridhishwa na matokeo ya awali yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo ambayo yalimpa ushindi mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi.

Tamko hilo kuhusu uchaguzi wa Congo lilitolea jana tarehe 17 Januari 2019 na viongozi wa A.U walipokutana mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Kufuatia tamko hilo, AU inaungana na Kanisa Katoliki nchini Congo ambalo pia lilipinga matokeo hayo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Tshsekedi kwa asilimia 38.5 ya kura akichuana kwa ukaribu na Martini Fayulu aliyepata kura asilimia 34.7, wakati mgombea aliyewakilisha muungano wa serikali, Emmanuel S hadary akiambulia asilimia 23.8.

error: Content is protected !!